Upandaji wa teff kwa safu hupunguza gharama ya pembejeo na kuongeza mavuno, hata hivyo kabla ya kupanda tayarisha shamba vizuri na lisawazishe.
Upandaji wa Teff kwa safu una faida kadhaa ambazo ni pamoja na; kuokoa mbegu, kusababisha ukuaji bora wa mimea, ni rahisi kudhibiti magugu na wadudu waharibifu, huongeza mavuno na kuokoa pesa.
Nyenzo za kutumia
Panda mbegu 3-5 za teff kwa hekta, kuwa na vijiti vya mbao, kamba, kijiti cha urefu wa 20cm, mbolea ya DAP na Urea kwa kiwango kinachopendekezwa kwa hekta. Funga kamba kwenye vijiti na simika vijiti ardhinini kwa upande mwingine na muachano wa 20cm kati ya safu. Tengeneza mitaro 3 – 4 kwenye safu, weka mbolea ya DAP na kuifunika na udongo kidogom. Chimba mashimo ya kupanda mbegu kwenye safu na zifunike kwa udongo wa cm 2 -3, kwani udongo mwingi utazuia mbegu kuota. Zao linapokuwa kwenye kimo cha kifundo cha mguu, weka kilo 50 za urea kwa hekta na vivyo hivyo baada ya mwezi 1.