Usimamizi wa mazao
Funika kitalu na matandiko ili kuzuia ndege kutoa mbegu. Nyunyizia maji shambani mara 3 wakati wa kiangazi. Vuna ngano kwa kukata mimea ukitumia kisu maalu, funga mimea kwenye vifungu na uvitandaze ardhini. Funika vifungo kwa kutumia kitambaa ili mbegu ziweze kuiva na kukauka vizuri.
Vile vile, baada ya wiki chache, ondoa nafaka kutoka kwa vibandazipepete kwa kutumia upepo. Kwa mwaka ujao, changanya mbegu zilizovunwa na mbegu zilizobaki katika msimu wa kwanza.