Matunda ya papai ni muhimu kwa wakulima, wafanyabiashara na walaji kwani ni vyanzo vya vitamini. Hizi kawaida hupandwa kwa kutumia viriba au kwenye kitalu.
Wakati wa mchakato wa kupanda, weka mbegu 4–5 kwa kila kiriba kwenye kina cha sm 1 na kisha nyunyizia maji yaliyochanganywa na dawa ya klorini. Viriba vinapaswa kuwekwa kwenye ardhi iliyoinuliwa na upandikizaji wa miche ufanyike baada ya wiki 8 – 10.
Wakati wa kuvuna tumia jukwaa lililoinuka ambalo hurahisisha kazi. Weka papai yaliyovunwa kwenye safu moja wakati wa kufungasha ili kuepuka kuharibu matunda.
Kupanda na kuhifadhi
Mwanzoni, lima ardhi mara 2 ili kulainisha udongo na kuchanganya nyenzo za kikaboni udongoni. Kisha tumia jembe linalozunguka kwa ukuaji sahihi wa mimea. Kisha tengeneza mitaro au matuta yaliyo na urefu wa cm 50 – 75 kando ya vitalu huku ukiacha umbali wa mita 4 kati yao ili kuboresha utiririkaji wa maji na kudhibiti uozo wa mizizi.
Pandikiza miche kwa umbali wa mita 1.5 hadi 1.8 na kisha ng‘oa miche ya ziada baada ya kuchanua maua ili kupunguza ushindani wa virutubisho.
Yanapokomaa vuna, safisha, ainisha na uweke lebo kwenye mapapai mara moja au mbili kwa wiki. Weka bidhaa kwenye masunduku, juu ya mbao kwa usafirishaji na uhifadhi rahisi. Hata hivyo, weka bidhaa kwenye chumba baridi ili kudhibiti upotezaji wa ubora.