»Kupanda pilipili. Jinsi ya kupanda, kukuza na kuvuna pilipili. 2/2 «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=tdJe-kWvou8&list=RDCMUCOL8wsKTTsgkAiLGzcT-Gdg&index=26

Muda: 

00:04:01
Imetengenezwa ndani: 
2014

Imetayarishwa na: 

infoagrocom

Kwa kuwa ni zao muhimu na lenye lishe, kilimo cha pilipili na uzalishaji wake hutegemea aina ya teknolojia inayotumika, ambayo huathiri ubora na wingi wa pilipili.

Pilipili hupandwa kwenye vitalu katika mwezi wa Februari na Machi, na hupandikizwa miezi 2 baadaye kwenye udongo unaofaa. Mmea huhitaji mwanga na joto la kutosha, pamoja na unyevu wa 50% –70%.

Kupanda pilipili

Miche hupandwa kwa muachano wa sm 40–50 ndani ya safu, na sm 60–70 kati ya safu. Pilipili hustawi katika udongo tifutifu ulio na mboji. Hata hivyo, muachano wa kawaida ni 1m x 0.5m lakini huu unaweza kupunguzwa hadi mimea 3 kwa kila mita ya mraba.

Vile vile, kumwagilia kunapaswa kufanywa ipaswavyo, na hivyo umwagiliaji kwa njia ya matone ni bora zaidi. Kutengeneza matuta huimarisha mimea na huhimiza ukuaji wa mizizi. Kusimamisha mimea pia kunafanywa ili kuepusha mimea kuanguka.

Kushughulikia pilipili

Wakati wa kupogoa, idadi ya mashina hupunguzwa hadi 2–3, na majani yenye ugonjwa huondolewa. Mwishoni mwa kipindi cha uzazi, ondoa vijicho vyote ili kuhimiza ukomavu, na pia ondoa matunda yoyote ambayo yanatokea chini ya shina la mmea. Hii ni kuhakikisha aina ya matunda ni ya ubora wa juu, na yana umbo bora.

Zaidi ya hayo, mpilipili huhitaji nitrojeni katika hatua za ukuaji za kwanza, wakati fosforasi huwa ni muhimu wakati maua ya kwanza yanapoonekana na katika mchakato wa kukomaa. Potasiamu inahitajika ili kutolea matunda rangi na ubora, wakati magnesiamu huwa ni muhimu katika hatua ya ukomaavu.

Wadudu waharibifu wa pilipili ni pamoja na inzi weupe na chawa, ambayo hudhibitiwa kwa njia ya kibiolojia kwa kutumia wadudu wenye manufaa. Magonjwa makuu ni pamoja na uozo, mnyauko na upele wa bakteria.

Hatimaye, uvunaji hutegemea aina zilizopandwa, na hali ya hewa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:23Pilipili hupandwa kwenye vitalu , na hupandikizwa kwenye udongo unaofaa.
00:2400:36Miche hupandwa kwa muachano wa sm 40–50 ndani ya safu, na sm 60–70 kati ya safu.
00:3700:43Mmea huhitaji mwanga na joto la kutosha, pamoja na unyevu halisi.
00:4400:51Pilipili hustawi katika udongo tifutifu ulio na mboji.
00:5201:03Muachano ufaao wa kawaida ni 1m x 0.5m lakini huu unaweza kupunguzwa hadi mimea 3 kwa kila mita ya mraba.
01:0401:13Kumwagilia kunapaswa kufanywa ipaswavyo.
01:01401:33Kutengeneza matuta huimarisha mimea na kuhimiza ukuaji wa mizizi.
01:3402:06Kusimamisha mimea pia kunafanywa ili kuepusha mimea kuanguka
02:0702:11Wakati wa kupogoa, idadi ya mashina hupunguzwa hadi 2–3.
02:1202:33Majani yenye ugonjwa huondolewa. Pia, majani au machipukizi yaliyo chini ya shina huondolewa.
02:3402:51Ondoa matunda yoyote ambayo hutokea chini ya shina la mmea.
02:5203:12Mpilipili huhitaji nitrojeni katika hatua za ukuaji za kwanza.
03:1303:17Fosforasi ni muhimu wakati maua ya kwanza yanapoonekana na katika mchakato wa kukomaa.
03:1803:26Potasiamu na magnesiamu huhitajika ili kutolea matunda rangi na ubora katika hatua ya kukomaa.
03:2703:30Wadudu waharibifu wa pilipili ni pamoja na inzi weupe na chawa.
03:3103:39Wadudu hudhibitiwa kwa njia ya kibiolojia kwa kutumia wadudu wenye manufaa.
03:4003:46Magonjwa makuu ni pamoja na uozo, mnyauko na upele wa bakteria.
03:4703:55Uvunaji hutegemea aina zilizopandwa, na hali ya hewa.
03:5604:01Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *