»Kupanda Soya«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=wWyLBESWznA

Muda: 

00:11:24
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

CABI

Kuchagua mbegu bora, kuchanja mbegu na aina zinazofaa za rhizobia, kuacha umbali sahihi kati ya mimea, na kuweka mbolea ni muhimu ili kufanikiwa katika upandaji wa soya.

Baada ya kuandaa shamba, hakikisha kwamba unapata mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wauzaji wa pembejeo, au kutoka kwa nafaka zilizohifadhiwa kutoka msimu uliopita iwapo huna uwezo wa kununua mbegu. Lakini iwapo unatumia nafaka zilizohifadhiwa zibadilishe kila baada ya miaka 3 ili kudumisha usafi wake. Pima uotaji wa mbegu siku 15 kabla ya kupanda, na chanja mbegu wakati wa kupanda.

Utaratibu

Mimea ya soya imethithiri rizobia ambayo huweka nitrojeni kwenye udongo. Kwa hivyo, ni bora kupanda nafaka katika msimu ujao baada ya soya. Kuweka chanjo ni nafuu kuliko kununua mbolea ya urea na kupaka rhizobia. Weka kilo 15 za soya kwenye chombo cha plastiki na ufunike, ongeza vifuniko 6 vya chupa vya maji ili kulainisha mbegu. Kisha ongeza 75g ya chanjo na uchanganye. Funika chombo na ukiweke kwenye kivuli kwa muda wa saa moja ili kukausha mbegu. Panda mbegu ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya kuweka chanjo. Hakikisha uko tayari kupanda mbegu kabla ya kuchanja.

Panda soya wakati mvua inanyesha, ambapo udongo una unyevu wa kutosho. Panda asubuhi au jioni ili kuepuka jua ya moja kwa moja kwa sababu inaweza kuharibu chanjo. Panda kwenye safu au mstari ulionyooka, kwa umbali wa 60cm kati ya safu na 5 cm ndani ya safu huku ukipanda mbegu moja tu kwa kila shimo. Kwa umbali wa 60cm x 10cm, panda mbegu 2 katika kila shimo.

Kupanda mseto kunaweza kufanywa na zao la nafaka, lakini kwa vile soya haistawi vyema kwenye kivuli, panda kwenye ukanda. Kupanda mseto kunaweza pia kufanywa katika mihogo mipya iliyostawi.

Kuongeza nitrojeni nyingi huzuia utengeneshaji wa Nitrojeni ya Kibayolojia, na piahuhimiza ukuaji wa majani. Fosforasi huongeza mavuno kwa kuhimiza ukuaji wa mizizi na vinundu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:03Andaa shamba, changua mbeg zilizoidhinishwa kutoka kwa wauzaji wa pembejeo.
01:0404:21Lakini Iwapo unatumia nafaka zilizohifadhiwa zibadilishe kila baada ya miaka 3. Pima uotaji wa mbegu.
04:2205:33chanja mbegu wakati wa kupanda.
05:3407:34Hatuaya kuchanja mbegu
07:3508:37Panda kwenye safu au mstari ulionyookawa, wakati wa mvua.
08:3809:24Panda kwenye safu, kwa umbali wa 60cm kati ya safu na 5 cm ndani ya safu
09:2511:12Panda mseto na zao la nafaka au katika mihogo mipya iliyostawi.Ongeza fosforasi.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *