»Kupandikiza mpunga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=BomO2rDg25M

Muda: 

00:14:17
Imetengenezwa ndani: 
2012

Imetayarishwa na: 

africaricecenter

Mavuno ya mchele ni mengi barani Afrika. Hata hivyo, mavuno yanaweza kuzidishwa iwapo wakulima watazingatia kanuni bora za usimamizi wa mpunga.

Kuna faida mbalimbali za kupandikiza mpunga ambazo ni pamoja na; kusababisha ukuaji wa haraka wa mimea, kurahisisha kupalilia kwa mazao, kuongeza mavuno, kutumia mbegu chache katika upanzi, na kuharakisha mchakato wa kuchagua mbegu. Hata hivyo, wakulima wanapaswa kupanga mapema shughuli za shambani kabla ya kupandikiza. Daima pandikiza miche kwenye kina cha 3cm kwa ajili ya kuotesha mizizi haraka, na hivyo kusababisha ongezeko la mavuno.

Shughuli za shambani

Hakikisha unatumia mbegu bora ili kupata miche yenye nguvu, lakini usipande mbegu nyingi kwenye kitalu kwani huku kunaweza kusababisha uotaji wa miche miembamba, ambayo itachukua muda mrefu kustawi vyema ili kupandikizwa.

Pia tayarisha shamba mapema kwa kusawazisha, na kulainisha udongo ili kurahisisha kupandikiza. Pandikiza siku 15–20 baada ya kupanda mbegu, wakati miche ina nguvu.

Hakikisha kuna kiwango kidogo cha maji kabla ya kupandikiza. Mwagilia kitalu kabla ya kung‘oa miche ili kupunguza uharibifu wa mimea.

Baada ya kung‘oa, pandikiza miche kwa haraka ili kuzuia miche kukauka. Hakikisha kwamba unapanda miche 1–3 kwa kila kilima ili kutoa matawi zaidi.

Daima hakikisha muachano ufaao kati ya mimea ili kurahisisha kupalilia na kuongeza mavuno.

Hatimaye, panda upya ndani ya wiki moja katika mahali ambapo mbegu hazikuota ili kuhakikisha ukuaji sawa wa mimea.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:47Mavuno yanaweza kuzidishwa iwapo wakulima watazingatia kanuni bora za usimamizi wa mpunga.
01:4802:04Faida za kupandikiza mpunga
02:0503:19Ukuaji wa haraka, kurahisisha kupalilia kwa mazao, kuongeza mavuno, kutumia mbegu chache katika upanzi, na kuharakisha mchakato wa kuchagua mbegu.
03:2003:28Hatua za kushughulikia katika kupandikiza mpunga.
03:2904:19Tumia mbegu bora, lakini usipande mbegu nyingi kwenye kitalu.
04:2005:46Tayarisha shamba mapema. Pandikiza siku 15–20 baada ya kupanda mbegu.
05:4706:16Tayarisha shamba mapema.
06:1706:41Hakikisha kuna kiwango kidogo cha maji kabla ya kung‘oa na pandikiza miche.
06:4208:44Baada ya kung‘oa, pandikiza miche kwa haraka kwenye kina cha 3cm.
08:4510:12Panda miche 1–3 kwa kila kilima.
10:1311:46Hakikisha muachano ufaao kati ya mimea. Panda upya ndani ya wiki moja katika mahali ambapo mbegu hazikuota.
11:4714:17Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *