Ili kupanua uzalishaji wa kuku, fuata miongozo kadhaa. Kufuga kuku kuna faida sana.
Nunua kuku kwenye soko la kienyeji. Ni bora kununua kuku wa kienyeji. Kabla ya kununua kuku, angalia sifa zake zifuatazo; Je! Kuku ni mzima na ana nguvu? Mkundu wake ni safi kwani kuku haharishi umaji umaji? Nunua kuku ambao hawajawahi kutaga mayai. Hakikisha unachanja kuku dhidi ya magonjwa makuu.
Uzalishaji wa vifaranga
Kuku mchanga anaweza kutoa mayai baada ya kutimiza umri wa miezi mitano. Halafu, hapo anaweza kuendelea kutoa mayai kwa muda wa miaka 2 hadi 3. Unaweza kutambua kuku ambaye amewahi kutaga mayai, kwa sababu tumbo lake huwa nzito na ngumu. Ni muhimu usiwe na jogoo wengi (jogoo mmoja kwa kuku 9) kwa sababu wao hupigania kutawala. Hii husababisha uzalishaji wa mayai machache.
Mara kuku anapotaga, hukaa juu ya mayai yake kwa siku 22 hadi 23. Hata baada ya mayai kuanguliwa, vifaranga huhitaji joto la mama yao. Katika wakati huu, kuku hatoi mayai zaidi.
Kufuga kuku
Ikiwa una familia kubwa au unataka kufanya biashara, unaweza kununua kuku zaidi. Jogoo mmoja huwatosha hadi kuku 9.
Baada ya kuleta kuku wako nyumbani, unafaa kuandaa chumba cha daraja mbili ambapo unaleta kuku kwa usiku. Katika daraja ya juu, weka vifaranga na daraja ya chini uweke kuku. Hakikisha kwamba unasafisha chumba cha kuku kila baada ya wiki mbili.
Walishe kwa mchele, mahindi, shayiri na semolina. Ikiwa una kuku wanaoatimia au kulalia mayai, weka chakula na maji karibu nao. Baada ya siku 8, kagua mayai ukitumia tochi ili uone ikiwa yai limerutubishwa. Wakati vifaranga wameanguliwa, watenganishe na mama yao baada ya siku 7 wakati wa joto, na baada ya siku 14 wakati ni kibaridi.