Uzalishaji wa vitunguu
Kwa sababu vitunguu hushambuliwa sana na magonjwa wakati wa mvua. Panda kwenye vitalu vilivyoinuliwa na kwa nafasi nzuri ili kudumisha afya ya mimea. Panda aina ya vitunguu inayokomaa ndani ya muda mfupi.
Vile vile, kaushia vitunguu shambani kabla ya kuvuna, na kausha vitunguu vilivyovunwa kwa siku chache kabla ya kuvihifadhi. Hifadhi vitunguu katika sehemu yenye baridi ya kutosha.
Hatimaye, safirisha vitunguu sokoni ili kupata bei nzuri.