Wakulima wanapaswa kuvuna vitunguu kwa uangalifu ili kudumisha na kuimarisha ubora wavyo. Ubora wa vitunguu unapopungua, bei ya sokoni pia hupungua.
Ni muhimu sana kutambua ishara za ukomavu sahihi na kuvuna katika wakati sahihi. Ishara hizi ni pamoja na vituungu huanza kuonekana juu ya ardhi, udongo ulio karibu na mmea hupasuka, ncha za majani hukauka, majani huanza kunyauka na kudondoka. Uvunaji hufanywa ama kwa mauzo ya mara moja (siku 70 hadi 80 baada ya kupandikiza) wakati ukubwa wa vitunguu ni gramu 70 hadi 90 au kwa kuhifadhi. Huku kunafanywa kutokana na bei ya chini iliyo soko, na kutunza ugavi wa vitunguu sokoni.
Mchakato wa kuvuna
Vitunguu bora vinapaswa kuwa na uimara mzuri, ngozi ya nyama iliyoshikamana, saizi na rangi inayofaa, harufu nzuri, bila uharibifu wowote. Uvunaji unaweza kufanywa kwa kutumia mikono au majembe madogo. Uvunaji wa mapema hufanywa kwa kutumia mikono wakati majani bado ni mabichi au yamekauka kiasi. Uvunaji wa kuchelewa hufanywa kwa kutumia majembe madogo wakati majani yamekauka. Baada ya kuvuna, kusanyia vitunguu chini ya kivuli na vitandaze ili kuepuka ongezeko la joto.
Kisha kata majani kwenye eneo la shingo huku ukiacha cm 1–2 ili kuzuia maambukizo na kuepuka kukauka kupita kiasi.
Mbinu za usimamizi baada ya mavuno
Kwanza sitisha kumwagilia ili kusaidia kuunda majani magumu ambayo hupunguza upotevu wa maji kutoka kwa majani ya ndani. Kisha hifadhi vitunguu chini ya kivuli kati ya nyuzi 27 – 30 kwa muda wa siku 5 hadi 10 ili kurefusha maisha ya vitunguu vilivyovunwa. Hata hivyo, epuka kuvikanyaga, kuvipakia kupita kiasi ili kuepuka uharibifu.
Pili, shughulikia na fungasha vitunguu kwa uangalifu ili kupunguza uharibifu. Safirisha vitunguu ukutumia vyombo vikubwa. Wakati wa kuhifadhi, ondoa nyezo zisizofaa na vitunguu vilivyoharibika. Ainisha vitunguu, na kisha vihifadhi kwenye jukwaa lililoinuliwa katika chumba kikavu ambacho kinaingiza hewa vizuri, huku ukizingatia usafi chumbani. Hakikisha paa halivuji, na pia fuatilia pamoja na kuondoa vitunguu vilivyooza na vilivyoshambuliwa.