Kutayarisha unga wa ndizi

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/making-banana-flour

Muda: 

00:11:45
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

KENAFF, Farm Radio Trust Malawi, UNIDO Egypt, Farmers Media Uganda

Unga wa ndizi hutayarishwa kutoka kenye ndizi mbichi zilizovunwa au kununuliwa. Unga wa ndizi unaweza kuishi kwa muda bila kuharibika kuliko ndizi mbichi, na unaweza kutumika kwa njia nyingi. Bei nzuri inaweza kupatikana na unga huo.

Unga wa ndizi hutumika kwa bidhaa kama vile uji, chapati, keki na ugali.

Jinsi ya kutayarisha unga wa ndizi

Vuna ndizi au nunua tu. Osha ndizi ili kuondoa uchafu wowote.

Katakata ndizi kwa vipande vidogo. Usiondoe maganda ili usipoteze virutubishi.

Kausha vipande hivyo katika eneo la kukaushia kwa siku 3 hadi 5. Kuwa makini na kudumisha usafi.

Pindua vipade vilivyo katwakatwa kila siku ili vikauke vizuri, hadi vitakapopasuka kwa urahisi.

Kusanya na uchukue vipande vilivyokaushwa kwa mashini ya kusaga, na uvisage kwa unga.

Kujaza na kuhifadhi

Pakia unga kwenye mifuko au vyombo visivyopenyeza hewa.

Hifadhi unga huo katika mahali pakavu. Unga wa ndizi unaweza kuishi kwa muda bila kuhariba kuliko ndizi kavu.

Vipimo kwa kiwango kinachohitajika na wateja vinaweza kufanywa.

Unga wa ndizi una manufaa nyingi kama vile virutubishi na fedha.

 

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:34Ndizi ni hasa chanzo cha mapato na chakula kwa familia nyingi.
0:3501:08Ndizi inaweza kubadilishwa kuwa unga.
01:0901:57Manufaa za kutayarisha unga wa ndizi: Usafirishaji rahisi, nafasi ndogo ya kuhifadhi, kukaa mda mrefu bila kuharibika , na unauzwa sana.
01:5804:31Unga wa ndizi una virutubishi sana
04:3205:17Vuna ndizi safi, zilizo na kijani kibichi, zisizo na kemikali au dawa.
05:1806:25Osha ndizi, toa uchafu wowote, kata ncha zote mbili.
06:2608:09Katakata ndizi kwa vipande vidogo na uzikaushe kwa jua
08:1009:12Pakia na uchukue kwa kusaga.
09:1309:43Kukusanya na kuhifadhi.
09:4411:45Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *