Silaji ni malisho ambayo hutengenezwa kutoka kwa mimea yenye unyevu mwingi kama vile mahindi bila uingizaji wa hewa ndani ya ghala. silaji huwa tayari baada ya wiki 2–3 za kuhifadhiwa ndani ya ghala.
Hata hivyo, ghala la shimo linapaswa kuwa na kina cha mita 2.5, upana wa mita 5 na urefu wa mita 12 kwa ajili ya kuongeza uhifadhi wa malisho. Sehemu ya juu ya ghala la shimo linapaswa kuinuliwa juu ya ardhi baada ya kulijaza na kulikandamiza. Silaji bora inapaswa kuwa ya kijani, kahawia au rangi ya dhahabu na sio nyeusi.
Hatua
Kwanza, tandaza lishe ya kijani kibichi katika safu na uikate katika vipande vidogo vya 5–10 cm. Fanye kila safu ya lishe iwe na unene wa cm 30–60. Kandamiza kila safu ili kuondoa hewa.
Kisha ongeza molasi au sukari guru kwa kiwango cha 3.5–4.0% ya uzito wa malisho ili kuboresha silaji na ladha yake.
Ongeza nafaka kwenye lishe. Ili kuweka nitrojeni nyunyizia urea kwenye silaji kwa kiwango cha 0.5–1% na ongeza chokaa kwa kiwango cha 0.5 hadi 1% ili kuongeza uzalishaji wa asidi.
Funika sehemu ya juu ya silaji kwa damani ya plastiki, kisha ongeza juu yake udongo wa kina cha inchi 6. Ondoa sehemu ambazo zinaweza kuingiza hewa na maji ili kudhibiti uharibifu wa silaji.
Hatimaye, tumia ghala mahsusi ili kutengeneza silaji juu ya ardhi.