Mwarobaini na kitunguu saumu ni viambato vya asili ambavyo vinaweza kutumika kutengeneza dawa bora ya kikaboni. Ili kutengeneza dawa kutoka kwa majani ya mwarobaini na vitunguu saumu, unahitaji kwanza kumenya vitunguu saumu na kuosha majani ya mwarobaini kwa maji.
Kutengeneza mbolea ya kikaboni
Baada ya kumenya vitunguu saumu na kuosha majani ya mwarobaini, viweke kwenye blenda au viponde kwenye kinu ili kutengeneza mchanganyiko.
Mimina mchanganyiko kwenye chombo na uuchujie kwenye chombo kingine.
Mimina mchanganyiko uliochujwa kwenye chupa ya dawa na ongeza maji. Baada ya hayo, mchanganyiko huwa tayari kutumika, lakini inashauriwa kunyunyizia dawa asubuhi au jioni wakati hali ya joto iko poa.