Kutengeneza mboji bora kunaweza kufanywa na mkulima yeyote. Unachohitaji ni taka ili kutengeneza mbolea oza au mboji. Taka zinazotumika hupatikana kutokana na mabaki ya matunda kama mananasi na maganda ya embe yote yakichanganywa pamoja.
Viungo vingine ni kutoka kwa maganda ya mananasi, maranda ya mbao na samadi ya kuku. Haya yote huchanganywa pamoja na hurundikwa. Ikiwa nyenzo za mboji zinajumuisha zilizonyevu na kavu, nyenzo kavu huwekwa chini kwanza kisha nyenzo nyevu huwekwa juu. Hii husaidia nyenzo kavu kupata unyevu kutoka kwa nyenzo nyevu. Viungo tofauti hutoa viumbe hai vidogo kutoka vyanzo tofauti, na hivyo kuzalisha mboji bora.
Kuozesha mchanganyiko wa nyenzo
Kuharakisha uozo wa nyenzo za mbolea hufanywa kwa kuongeza chachu au kichochezi. Iwapo huna kichochezi, kata vifaa katika vipande vidogo ili viweze kuoza haraka.
Inachukua miezi 2–3 kwa mchanganyiko kuwa tayari kikamilifu. Katika kipindi hicho, mkulima anapaswa kufanya yafuatayo; kugeuza mchanganyiko mara kwa mara ili kuondoa hewa na kueneza viumbe vidogo. Kuongeza nyenzo kavu zaidi ili rundo liweze kupata joto au kuongeza nyenzo za kijani wakati rundo linapoaza kupata joto zaidi.
Viumbe hai zaidi
Mbole ya maji ya minyoo hutengenezwa kutoka kwenye mboji kwa kuweka mboji kwenye gunia na kuitumbukiza kwenye maji. Vijidudu na virutubishi vilivyo kwenye udongo huingiya polepole ndani ya maji na mchakato huchukua kati ya siku 7–10. Kisha mbolea hutolewa nje na na mbolea ya maji huchanganywa na kutumiwa.
Mbolea ya maji husaidia mimea kustahimili magonjwa na pia kustahimili ukame. Kwa kawaida mbolea ya maji hunyunyiziwa kwenye majani ya mmea.
Kuweka mboji
Mbolea kawaida huwekwa kati ya mimea, juu ya udongo karibu na mmea. Mbolea hutoa harufu nzuri ikiwa tayari.
Kwa kilimo cha majani, kutengeneza mboji ni njia bora ya kutumia tena taka zilizotengenezwa shambani.