Takataka zinazotokea shambani mwako au kutoka kwa viwanda vya usindikaji zinaweza kubadilishwa kuwa mbolea kwa kiwango kidogo, kiwango cha wasitani au kikubwa. Mbolea oza ni muhimu katika kilimo.
Mbolea oza hutolea mimea virutubisho, na pia huongeza mboji kwenye udongo ambayo husaidia udongo kuhifadhi maji, hupunguza gharama za kununua matandazo ya plastiki.
Mchakato wa kutengeneza mboji/ mbolea oza.
Ili kutengeneza mboji, unahitaji nyenzo ambazo ni pamoja na taka kutoka kwa viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo, pumba za mbao, samadi ya kuku. Ongeza kichocheo ambacho huharakisha mchakato, au waweza pia kukatakata nyenzo katika vipande vidogo.
Runda nyenzo ukianza chini na zilizokauka, zile ambazo hazijakuaka huwekwa juu. Inachukua kati ya miezi miwili hadi mitatu kwa mbolea oza kuwa tayari, lakini katika muda wa miezi mitatu, geuza mchanganyiko mara kwa mara kwa kutumia mashine kutegemea na wingi wake.
Wakati mboji iko tayari, iweke kwenye udongo karibu na mmea au itumie kutengeneza mbolea ya maji kwa kuweka mbolea oza kwenye mifuko na kuitumbukiza kwenye maji kwa muda wa siku 7 hadi 10. Virutubisho huchuja polepole ndani ya maji, na kisha maji haya huwekwa kwenye mimea. Mbolea ya maji husaidia mimea kustahimili magonjwa na ukame.