Mmomonyoko wa udongo kwenye mteremko ni jambo la kawaida, na husababisha upotevu wa virutubisho vya mimea. Mianzi inaweza kutumika kudhibiti mmomonyoko wa udongo.
Katika usimamizi endelevu wa ardhi, udhibiti wa mmomonyoko wa udongo ni muhimu hasa kwa maeneo yenye mazingira duni. Mwanzi unaweza kuenezwa kupitia kizizi. Ili kuzidisha mwanzi, chimba kizizi cha mianzi ambao umechipuka na ukipandikize moja kwa moja kwenye shamba au kwenye kitaul/ viriba.
Njia zingine za kueneza mianzi
Mwanzi pia unaweza kuenezwa na vipandikizi vilivyopatikana kutoka kwa miti ya mianzi ambayo ni angalau miaka 3. Kata vipandikizi vilivyo na angalau vifundo 2, kwa pembe ya digrii 45, na ondoa sehemu za mmea zilizochipuka. Baada ya wiki 8 hadi 10, mche huanza kustawi na baada ya hapo, unaweza kuupandikiza.
Unaweza pia kueneza mianzi kwa kutumia kizizi kukuu.
Faida za mianzi
Panda kichaka kimoja au viwili vya mianzi kwenye ardhi iliyoteremka ili kudhibiti mmomonyoko. Hii ni njia bora kwa mazingira ya kudhibiti mmomonyoko wa udongo. Mianzi haihitaji utunzaji mwingi, kwa hivyo, mara tu inapopandwa, inaweza kukua peke yake.
Mianzi pia inaweza kutumika katika viwanda vya mbao, utengenezaji wa karatasi, kutumika kama nyenzo ya ujenzi na kutengeneza vitalu. Mianzi kwa matumizi ya viwandani unapaswa kuwa na angalau umri wa miaka 5.