Mmomonyoko wa udongo huwa mwingi katika maeneo yenye mteremko. Mistari ya nyasi iliyopandwa kando ya mtaro (contour) hupunguza kasi ya maji yanayotiririka , na kuruhusu maji yapenyeze kwa udongo na hivyo, kusaidia kudhibiti mmomonyoko. Na pai, hushikilia udongo na viritubisho vilivyo kuwa vimesombwa kutoka juu.
Aina tofauti za nyasi zinaweza kutumika, lakini chagua aina ya nyasi isiyoshindana sana na mazao au kuzaa mbegu nyingi. Unaweza pia kuacha majani ya asili.
Uanzishaji wa nyasi
Mistari ya nyasi inaweza kuanzishwa kwa kutumia mbegu au kung’oa mabonge ya nyasi iliyokomaa. Katika safu moja, panda mistari 3 ya nyasi na kuacha nafasi ya takribani sentimita 20. Unapotumia nyasi zilizong‘olewa, kata nyasi hizo hadi 20cm na ugawanye mashina na mbegu hizo kabla ya kuzipanda. Tumia A frame kupima muinuko wa ardhi au mstari wa contour. Basi panda nyasi katika mashimo ya kina cha sentimita 10cm, acha nafasi ya sentimita 10–20 cm katikati , kisha panda mstari wa pili kando na ule wa kwanza huku ukihakikisha kwamba mashimo yanapitana. Acha nafasi ya mita 20 katika safu za nfasi zilizo kwenye mteremko mpole, na mita 10 kwenye mteremko mkali. Hakikisha kwamba hakutakuwa myanya kwenye safu za nyasi, kwa hivyo lazima zijazwe mwanzoni mwa msimu wa mvua. Nyasi zinaweza kuvunwa kuwa chakula cha mifugo, na kutumika kuandaa chakula cha kuhifadhia mifugo (silage), na kulisha samaki.