Kwa ardhi ndogo, chakula kinaweza kuzalishwa kwa kutumia vilima vya gunia. Kufanya hivyo, changanya udongo wa juu na mbolea oza kisha uyajaze katika gunia ukiweka mawe madogo katikati. Mboga za majani hupandwa pembeni ya gunia, na mboga za kusimamishwa hupandwa juu.
Vifaa vinavyohitajika: gunia, bomba la urefu wa 1m, udongo wa juu, mbolea oza, mawe madogo, vigingi, na miche ya mboga. Changanya vipimo viwili vya mchanga na kipimo kimoja cha mbolea oza. Jaza gunia na mchanganyiko huo hadi 15 cm. Weka bomba (pipe) katikati na uijaze na mawe madogo. Jaza eneo iliyokaribu na bomba na mchanganyiko wa udongo na mbolea. Chomoa bomba gunia litakapojaa. Imarisha gunia katika mahali moja kwa kutumia vigingi, na ukate mashimo madogo ya 2cm ukiacha nafasi ya 10cm baina ya mashimo haya. Mwagilia maji vizuri na upande juu ya gunia mboga zinazohitaji kusimamishwa, na mboga za majani zipandwe pembeni. kisha mwagilia maji baadae.
kurutubisha udongo
Tumia virutubisho asili vya mimea vilivyotengenezwa kwa kujaza chombo hadi robo tatu na majani mbichi yaliyokatwa. Ongeza maji, na ukoroge mara moja kila siku kwa siku 5. Nyunyiza mara moja kila wiki 2 kwa kuchanganya theluthi moja ya virutubisho asili vya mimea na theluthi tatu ya maji.