Mbuzi na kondoo hufugwa kutoa nyama, maziwa, ngozi na sufu. Shambulio la minyoo ni shida kubwa na huathiri ukuaji na ubora wa ngozi. Katika hali mbaya bila utunzaji mzuri, wanyama wanaweza pia kufa. Mbuzi walioshambuliwa na minyoo hawali, na kuharisha sana kunaweza kuwaua. Mbuzi walioathiriwa hawajichanganyi na wengine, wala hawatendi chochote na huharisha minyoo kwenye kinyesi chao.
Dalili na njia ya maambukizo
Tumbo huvimba na mnyama huharisha minyoo myeupe na harufu mbaya, mnyama hupunguza uzito, na tumbo lake huvimba. Minyoo ya vimelea huenea kupitia hali za uchafu, maji machafu na maeneo ya kulishia yaliyoshambuliwa. Minyoo kutoka kwa wanyama walioathiriwa huambukizwa kwa wale walio na afya wakati wa kulisha kupitia kwa majani na nyasi. Na kadhalika, kupitia wanyama wagonjwa hadi wanyama wenye afya wakifugwa katika banda/zizi moja.
Maandalizi ya dawa za minyoo
Mambukizi ya minyoo yanaweza kuzuiliwa na kuponywa kwa mitishamba ya asili. Changanya mwarobaini, mtukututu, majani ya mshubiri kwa usawa na kipimo kidogo cha maji. Kisha saga pamoja ili kutengeneza mchanganyiko.
Kinga: Wape wanyama mchanganyiko mara moja kila miezi mitatu ili kuzuia minyoo. Wape dawa mbuzi na kondoo kabla ya kushambuliwa na minyoo. Dawa inayopewa kabla wanyama hawajakula chochote hufanya vizuri.
Kipimo
Kijiko kimoja cha chai kinatosha kondoo na mbuzi zilizochini ya miezi mitatu. Unusu wa kikombe unatosha kwa mbuzi wazima mara moja kila miezi mitatu. Tumia dondoo la mitishamba katika siku mbili za maandalizi.
Uhifadhi
Weka dondoo kwenye chombo kisichopenyeza hewa. Kagua hali ya kinyesi cha wanyama iwapo kuna minyoo tena. Kama kuna minyo tayarisha upya mchanganyiko. Dawa halina athari mbaya, na ni rahisi kuwapa wanyama, na pia sio ghali kuandaa. Kamwe, usiwape dawa ya minyoo wanyama wajawazito kwani linaweza kusababisha utoaji wa mimba. Lisha wanyama baada ya kuwapa dawa ya minyoo ili waweze kuwa na nguvu, na afya.