Wanawake wengi barani Afrika wanapenda kuwafuga mbuzi kwa sababu ni rahisi kuwachunga hata kwenye kipande kidogo cha ardhi. Maziwa ya mbuzi huuzwa kwa bei ya juu sokoni, yana kiwango cha juu cha lishe, na pia ni mazuri kwa watoto pamoja na wazee.
Ili kutoa maziwa mengi, mbuzi wa maziwa wanahitaji kulishwa vizuri. Mbuzi waliolishwa vizuri hukua haraka na wana uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto, pamoja na kuzalisha maziwa zaidi. Malisho husaidia kukidhi baadhi ya mahitaji ya mbuzi kama vile nguvu, protini, vitamini, na madini. Malisho ni pamoja na nyasi, mabua ya mahindi na mabaki ya mazao, majani ya ndizi, na vichaka. Mashina ya ndizi yaliyokaushwa, migrivea, majani ya viazi tamu, majani ya mbaazi, na maharagwe husaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa. Vyanzo vingine vizuri vya protini ni pamoja na mabaki ya soya, unga wa samaki na keki ya mbegu za pamba, mabavyo mara nyingi hupatikana katika duka la vyakula vinavyonunuliwa. Lishe linapaswa kukaushwa kwa angalau siku 3 kabla ya kuwalisha mbuzi ili kuepuka kuharisha. Wape mbuzi maji safi kwa sababu maji husaidia mbuzi kumengenya lishe, na hivyo kuongeza uzalishaji wa maziwa.
Tahadhari kwa mbuzi wa maziwa
Ondoa chakula kilichobaki kutoka kwenye kihori cha chakula. Safisha vizuri kihori kabla ya kuweka chakula kingine kwa sababu mbuzi wanaweza kuwa wamekikojolea.
Chakula kinapaswa kuwekwa kwenye kihori kilichoinuliwa ili kuepuka kukichafua. Funika lishe iwapo mvua inataka kunyesha ili kibaki kavu. Epuka kuwalisha mbuzi mimea iliyo na sumu kwa sababu inaweza kusababisha uvimbe na kuua mbuzi. Changanya magadi na maji na uwape mbuzi ili kutibu uvimbe wa tumbo.
Epuka kuwalisha mbuzi vitunguu na majani ya sukumawiki kwa sababu yatasababisha maziwa kutoa harufu mbaya. Hifadhi lishe katika hali ya nyasi kavu ili kutumika wakati wa kiangazi.
Kiwango cha kuwalisha mbuzi
Wape mbuzi wa maziwa chakula kingi kadri wanapokua ili kudumisha afya nzuri. Iwapo mbuzi wana mimba, changanya chakula na mikono 3 iliyojaa lishe ya maziwa katika miezi 3 ya mwisho wa mimba ili kupata watoto wenye afya na maziwa mengi. Kwa mbuzi anayenyonyesha, ongeza mikono 3 ya lishe ya maziwa katika chakula ili kuendelea kutoa maziwa.