Kuzalisha mbegu za migomba zenye afya

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/producing-healthy-plantain-and-banana-suckers

Muda: 

00:13:55
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Access agriculture
Kwa vile upandaji wa migomba huhitaji mbegu, mbegu ya migomba ni mmea mdogo wa ndizi unaokua chini ya mmea mama.
Wakulima huchukua mbegu moja kwa moja kutoka kwa mmea mama, hata hivyo mimea mama mara nyingi hushambuliwa minyoo fundo, kuvu, na fukusi wa migomba. Sehemu ya migomba iliyo chini ya ardhi ambayo hujulikana kama kiini cha mbegu hutoa mizizi na machipukizi ambayo hukua na hubadilika kuwa shina.

Uzalishaji wa mbegu za migomba 

Kwanza, kuzidisha mbegu za kupandia, kuna hitaji la kifaa cha kuotesha, chafu (green house), kivuli na mbegu safi. Chagua mmea mama, ondoa mmea chipukizi wenye urefu wa mita 1 na majani membamba yenye umbo la mkuki. Usiondoe mimea iliyoelekea kwenye mwelekeo wa upepo mkali kwa vile inalinda mmea mama dhidi ya kuanguka. Ondoa kwa upole mmea na uukate tena kwa urefu wa sm 30. Kisha safisha mmea ukiwa bado shambani ili kuepuka kueneza magonjwa.
Vile vile, ondoa sehemu za kiini cha mbegu za nje sawa na 3-5 cm, pamoja na mizizi hadi mbegu iwe nyeupe kabisa na uondoe maganda ya majani kwenye msingi wa kiini cha mbegu huku ukiacha tu jani la kati kwani linaweza kuchipuka kabla mbegu haijatibiwa. Loweka kiini cha mbegu ndani ya dawa kwa dakika 10-15 na kisha ukikaushe kwa siku 2-3. Endelea kwa kuweka kiini cha mbegu kwenye sehemu safi chini ya  kivuli pasipo na jua wala mvua.
Baada ya kukausha, ondoa jani la katikati na ukate katikati la kiini cha mbegu. Kisha weka mbegu iliyotibiwa kwenye sanduku la kuoteshea lenye kina cha sentimita 50 lililowekwa kwenye eneo lililohifadhiwa vizuri, huku ukiliepusha kugusa udongo kwa kuongeza safu ya 10cm ya changarawe chini yalo. Ongeza safu ya majivu chini ya kisanduku ili kuua viini vilivyo kwenye udongo. Weka shimo la kuondoa maji kwenye kisanduku cha kuoteshea. Jaza kisanduku na machujo ya mbao, ondoa vipande vya mbao vilivyomu, ongeza maji safi, changanya vizuri, weka ndani mbegu za mgomba zikisimamishwa wima kwenye machujo ya mbao na uzifunike kwa machujo ya mbao yenye unene wa 3cm. Mwishowe, funika kisanduku na karatasi ya plastiki ili kuhifadhi unyevu ndani. Weka kivuli au paa la majani ya mitende, mwagilia maji siku inayofuata na kisha mara mbili kwa wiki. Hakikisha unakifungua kisanduku kwa dakika 5 kila siku.
Zaidi ya hayo, baada ya wiki 3-6, ondoa mbegu za migomba na uondoe majani yoyote yaliyokufa na na yale yenye madoa meusi. Mwagilia maji kwenye viriba vilivyojazwa na udongo na panda mbegu ndani yavyo. Hatimaye, pandikiza mbegu baada ya wiki 6-8.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:21Ili kupanda migomba, unahitaji mbegu.
00:2200:30mbegu ya migomba ni mmea mdogo wa ndizi unaokua chini ya mmea mama.
01:3102:05kuzidisha mbegu za kupandia, kuna hitaji la kifaa cha kuotesha, chafu (green house), kivuli.
02:0602:30Sifa nyingine ni na mbegu safi
02:3103:31Chagua mmea mama, ondoa mmea chipukizi wenye urefu wa mita 1 na majani membamba yenye umbo la mkuk
03:3203:39Usiondoe mimea iliyoelekea kwenye mwelekeo wa upepo mkali.
03:4004:03Ondoa kwa upole mmea na uukate tena kwa urefu wa sm 30.
04:0404:53safisha mmea ukiwa bado shambani. Ondoa sehemu za kiini cha mbegu za nje sawa na 3-5 cm.
04:5405:20Ondoa maganda ya majani yaliyo kwenye msingi wa mbegu, ukiacha tu lile la katikati.
05:2106:29Loweka mbegu kwenye viuatilifu kwa muda wa dakika 10-15 na kausha kwa siku 2-3.
06:3006:39Weka mbegu kwenye sehemu safi, chini ya kivuli pasipo na jua wala mvua.
06:4007:09aada ya kukausha, ondoa jani la katikati na ukate katikati la kiini cha mbegu.
07:1008:18weka mbegu iliyotibiwa kwenye sanduku la kuoteshea, huku ukiliepusha kugusa udongo.
08:1908:32Ongeza safu ya majivu chini ya kisanduku ili kuua viini vilivyo kwenye udongo. Weka shimo la kuondoa maji kwenye kisanduku cha kuoteshea.
08:3309:02Jaza kisanduku na machujo ya mbao, ondoa vipande vya mbao.
09:0309:23 ongeza maji safi, na changanya vizuri
09:2409:39weka ndani mbegu za mgomba zikisimamishwa wima kwenye machujo ya mbao na uzifunike kwa machujo ya mbao yenye unene wa 3cm.
09:4009:59funika kisanduku na karatasi ya plastiki ili kuhifadhi unyevu ndani. Weka kivuli au paa la majani ya mitende.
10:0010:19mwagilia maji siku inayofuata na kisha mara mbili kwa wiki. Hakikisha unakifungua kisanduku kwa dakika 5 kila siku.
10:2010:55aada ya 3-6, ondoa mbegu za migomba zilizoota.
10:5611:15Ondoa majani yoyote yaliyokufa na yale yenye madoa meusi kutoka kwa mbegu. Mwagilia maji kwenye viriba vilivyojazwa na udongo
11:1611:46panda mbegu ndani viriba hivyo.
11:4711:57Hatimaye, pandikiza mbegu baada ya wiki 6-8.
11:5813:55Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *