Kupogoa ni hatua ya kuchagua na kuondoa sehemu fulani za miti ili kuboresha afya yake na afya ya matunda.
Kupogoa hutoa miti midogo ambayo ni mifupi na ina matawi wazi, halafu miti ambayo haijapogolewa huwa na urefu wa angalau mita sita, na matawi mengi
Kubainisha miti iliyopogolewa na miti isiyopogolewa
Kupogoa humuwezesha mkulima kuwa na msongamano mkubwa wa miti shambani kulinganishwa na miti isiyopogolewa. Miti isiyopogolewa hupandwa kwa muachano wa mita 10 kwa 10 na hufanya shamba kuwa na idadi ndogo ya miti kulinganishwa na miti iliyopogolewa, ambayo hupandwa katika umbali wa 5m kwa 5m.
Miti isiyopogolewa hushambuliwa sana na magonjwa ya kuvu kama vile chule kwa kuwa matawi yao huchukua muda mrefu kukauka baada ya mvua, kulinganishwa na miti iliyopogolewa ambayo hukauka haraka baada ya mvua, kwa sababu ya mzunguko rahisi wa hewa na mwangaza wa jua.
Kukagua shamba ni hatua ya kwanza ya udhibiti mzuri wa magonjwa. Kufanya huku ni ngumu kwenye miti isiyopogolewa, kulinginishwa na miti iliyopogolewa.
Kunyunyizia dawa ya kuvu ni hatua nyingine muhimu katika udhibiti wa magonjwa. Ni rahisi kunyunyizia matawi yote bila kupoteza kemikali kwenye miti iliyopogolewa, lakini ni ngumu kwenye miti isiyopogolewa, na hivyo kuna upotezaji mwingi wa kemikali.
Maua katika miti iliyopogolewa hukua wakati huo huo iwapo ncha za matawi zimekatwa baada ya kuvuna, lakini kwenye miti isiyopogolewa, maua hukua nyakati tofauti.
Matunda zaidi huzalishwa kwa kila mti kwenye miti isiyopogolewa lakini maembe ya miti iliyopogolewa ni kubwa kulinganishwa na ya miti isiyopogolewa. Kwa ekari, miti iliyopogolewa pia hutoa mazao mengi kuliko miti isiyopogolewa.
Miti iliyopogolewa kwa ujumla hutoa mazao mengi, uzalishaji huwa uendelevu kwa muda mrefu, na hutoa matunda yenye ubora wa juu ambayo huiva sawiya.