Baada ya kulima, udongo mara nyingi huonekana umevunjika na unaweza kushambuliwa na jua au upepo. Kuzidisha kulima, ndio uharibifu wa ardhi zaidi.
Udongo mwingi humomonyoka kwa sababu ya mvua na upepo. Kabla ya kulima, udongo hufunikwa na mabaki ya mimea ambayo yanalinda shamba dhidi ya mmomonyoko. Mabaki ya mimea yakioza, hubadilika mbolea. Udongo ambao hujalimwa, mara nyingi huwa kavu.
Kilimo cha usumbufu uchache wa udongo
Ili kutunza udongo, usichome kitu shambani kabla ya kulima. Ikiwa kuna mabaki ya mimea mingi shambani, unaweza kuikatakata na panga ili urahisishe kufanya kazi.
Kwa kilimo cha usumbufu uchache wa udongo, unaweza kutumia trekta kidogo. Ni rahisi kutumia trekta mara ya kwanza, kisha ndio ulime mara kadhaa. Uwezekano mwingine wa kilimo cha usumbufu uchache wa udongo ni kutumia sub soiler ndogo. Hii ni nzito na huingia ndani ya udongo bila kugeuza bali kulainisha udongo.
Kulima cha kutolima chochote ‘‘zero tillage‘‘
Kilimo cha zero tillage kunamaanisha kuacha kabisa udongo bila kuulima. Unaweka tu mabaki ya mmea kwenye mistari na safu za mimea kati yao. Kwa hivyo, unaweza kutumia kijiti cha kupanda. Unapaswa kuweka umbali sawa na kiasi cha mbegu kama vile ungetumia kwa kulima.
Usipolima utakuwa na magugu zaidi, haswa katika mwaka wa kwanza. Kwa hivyo, ni muhimu kudhibiti magugu kwa dawa katika siku 25 za kwanza. Baada ya haya, mahindi yanaweza kujikinga.
Kilimo cha usumbufu uchache wa udongo na kilimo cha kuacha udongo kabisa bila kuulima husababisha matokeo bora. Katika mwaka wa tatu utagundua kuwa udongo una rutuba zaidi na huonekani umemomonyoka.
Kila baada ya miaka 5, udongo unakuwa ngumu na unafaa kulimwa. Ikiwa ng‘ombe huishi shambani mwako, unalima ili kulainisha udongo.