Usimamizi wa nyasi na malisho ya mifugo ni jambo kubwa katika ufugaji, na una fursa nyingi sana. Mafunzo kuhusu hili yanatolewa na mpango wa KSAP kwa watoa huduma kutoka bunge za Marsabit na Isiolo nchini Kenya.
Kwa ufugaji wa kibiashara, lazima uwe na ujuzi na maarifa juu ya usimamizi wa nyasi na malisho. Pia, mikakati ya kusaidi kupata nyasi na malisho kwa mwaka mzima inahitajika. Mafunzo juu ya mbinu za uanzishaji, uvunaji na ukadiriaji wa majani huwasaidia wafunzwa kuwa na uwezo wa kuwasaidia wakulima katika kukadiria ni kiasi gani cha kutarajia mwishoni mwa msimu.
Uboreshaji wa nyasi
Uboreshaji wa nyasi asili ni kwa kupanda aina bora za nyasi katika maeneo kame. Hii hufanywa kwa sababu ya upungufu wa mbegu za nyasi kutokana na mafuriko na mmomonyoko ambao hubeba mbegu.
Uwiano wa faida na gharama hutekelezwa ili kutambua mbinu bora miongoni mwa mbinu zote zinazotolewa kwa wakulima. Pia wakufunzi hufunzwa kuhusu jinsi ya kuwaeleza wakulima kwa njia rahisi zaidi.
Suluhisho zaidi
Wafugaji huamua kuuza mifugo yao kutokana na sababu mbalimbali kama vile ukame. Kwa hivyo mafunzo haya yanawafahamisha namna ya kutolazimika kuuza ng‘ombe wote kwa kuongeza hifadhi zao za malisho ambayo yatatumika katika msimu wa kiangazi.
Hii husaidia kuongeza uzalishaji, kwani wanyama huweza hustawi katika mazingira kama hayo, hivyo basi kupunguza hasara ambazo wangeweza kupata.