Mahindi yana aina nyingi na yanaweza kupandwa katika maeneo mbalimbali ya ikolojia ya kilimo. Kila sehemu ya mahindi ina thamani ya kiuchumi.
Kilimo cha mahindi
Daima fanya uchunguzi wa udongo kabla ya kupanda. Kusanya sampuli nzuri kwa kina cha 20cm na upeleke sampuli kwenye taasisi ya utafiti wa udongo kwa uchambuzi. Ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mahindi inaweza kutayarishwa kwa mikono au mashine kulingana na historia ya ardhi hiyo. Iwapo ardhi ina mteremko, lima kutoka upande moja wa mteremko hadi mwingine ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. Mbegu zinapaswa kuthibitishwa na kununuliwa kutoka kwa wauzaji wa pembejeo. Hatua ya kupima uotaji wa mbegu ifanyike kabla ya kupanda. Kupanda kunafanywa kwa kutumia mashine au mikono mwanzoni mwa msimu wa mvua, au wakati mvua inatarajiwa kunyesha kwa aina za mahindi zinazostahimili ukame. Wakati wa kupanda, weka mbolea kwa kina cha 10cm, kisha funika na udongo ili kutengeneza shimo la kina cha sentimita 5 ambamo mbegu hupandwa.
Udhibiti wa magugu
Udhibiti wa magugu unapaswa kufanywa mapema iwezekanavyo. Hilo hufanywa kwa kubadilisha mazao, kuacha nafasi sahihi kulingana na aina, kupanda kwa wakati, kupalilia na kungoa kwa mikono, kuweka mbolea na kutumia mbegu bora bila magugu. Kemikali pia zinaweza kutumika kudhibiti magugu.