Vimelea vimegawanywa katika makundi mawili: Vimelea vya nje na vya ndani. Vimelea vya nje huishi nje ya mwili wa mtu au mnyama.
Vimelea vya ndani huishi ndani ya mwili wa mnyama na hawaonekani. Wanaweza tu kutambuliwa kutokana na athari zao kwa wanyama. Aina tofauti za vimelea vya ndani ni minyoo na kosidia.
Minyoo
Kosidia ni vimelea vidogo ambavyo hukaa ndani ya matumbo ya nguruwe na huzuia matumbo kuingiza chakula.
Minyoo imegawanywa katika safuri, mchango duara, na tegu. Mchango duara humezwa kama mayai au mabuu kupitia vyakula vilivyochafuliwa na maji katika. Haya husababisha ubadilishaji duni wa chakula, na hivyo kusababisha ukuaji duni wa nguruwe.
Minyoo ya mapafu huziba mapafu, na hivyo kufanya nguruwe kukohoa mara kwa mara.
Minyoo tegu
Mwili wa tegu una sehemu kama kidole cha binadamu. Kila sehemu hukatika kadiri mnyoo anavyokua.
Minyoo ya tegu hunyonya damu kutoka kwa nguruwe na kuwafanya kuwa dhaifu. Nguruwe wanaposhambuliwa na minyoo hawakui, kinga yao huanza kushuka na kukabiliwa na upungufu wa damu.
Unaweza kupata minyoo au vipande vyake kwenye kinyesi cha nguruwe.
Kuzuia minyoo
Minyoo inaweza kupatikana kwenye tumbo. Hakikisha chakula na maji havijachafuliwa.
Tumia njia ya mrija na mabomba ili kunyweshea mifugo badala ya vihori vya maji ili kuwazuia nguruwe kuchafua maji. Katika hali ambapo mtu hawezi kumudu mrija na mabomba, tumia maji vihori vyembamba vya maji na chakula.
Wasiliana na daktari wa mifugo kwa miezi 2–3 ili wapewe dawa ya kuua minyoo mara kwa mara. Vimelea vya ndani hupatikana sana miezi 2–3 baada ya kuachisha nguruwe kunyonyesha.