Kupogoa ni mbinu kuu ya usimamizi katika miti ya matunda na miti ya misitu lakini wakulima wengi wanajiuliza ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kuchagua matawi ya kupogoa.
Wakati wa kuchagua matawi ya kupogoa, kwanza chunguza mti. Huku kunahusisha kuutazama mti na kufanya maamuzi fulani kuhusu mti, yaani jinsi mti ulivyo kiafya, kasi ya ukuaji wa mti, muundu wa mti, na aina ya miti.
Mambo mengine
Hatua moja muhimu wakati wa kutathmini na kuchunguza mti ni kutafuta tawi kuu ambalo hukua katikati ya mti.
Tafuta na kuondoa matawi duni ambayo ni pamoja na yale yaliyokufa, yaliyoharibiwa, yaliyoathiriwa na magonjwa. Haya yote lazima yaondolewe wakati wa kupogoa.
Pia angalia matawi yanayoshindana. Haya ni pamoja na matawi ambayo yanashindana na tawi kuu huku yakijaribu kulizuia kukua zaidi. Haya pia yanapaswa kuondolewa wakati wa kupogoa.
Ondoa au punguza matawi yanayoshindana ili kuwezesha tawi kuu ki kustawi vyema.