Kideri ni moja wapo ya magonjwa hatari ya kuku na unaweza kusababisha hasara kubwa ikiwa hautadhibitiwa.
Kideri ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na hauna matibabu ila unaweza kudhibitiwa tu. Kwa kawaida kideri hushiriki na magonjwa mengine kwa mfano ugonjwa mapafu. Udhibiti wa ugonjwa huu ni kwa kuanzisha shamba lako mbali na mashamba mengine, kuzuia wageni kuingia kwenye shamba lako, kuzuia mfadhaiko kwa ndege na kuchanja ndege kwa wakati sahihi.
Dalili za ugonjwa wa kideri
Kuna aina 3 za ugonjwa wa kideri. Aina ya kwanza (lentogenic), ambayo sio kali sana, na mara nyingi husababisha dalili kidogo za kupumua kwa mfano kikohozi na dalili zingine kama vile kuhara kinyesi cha kijani kibichi.
Kuna aina ya pili (mesogenic), ambayo ni hatari kuliko ya kuanza, na hupunguza uzalishaji wa mayai.
Aina ya tatu ya ugonjwa ni hatari zaidi na inaweza kusababisha karibu asilimia 80 ya vifo ndani ya siku 3 na inahusisha dalili kama vile uharibifu wa mfumu mkuu wa mishipa, kupinda shingo na ndege kuyumbayumba wakitembea.
Kudhibito ugonjwa wa kideri
Ili kudhibiti ugonjwa wa kideri, ongeza kingamwili za ndege kwa kuondoa mambo yoyote yanayosababisha mafadhaiko. Wape ndege vitamini nyingi hasa vitamini C kwa sababu hizi hupunguza mafadhaiko.
Tibu maambukizi yote, na uwape ndege chakula bora.