Kupanda mbegu duni husababisha mimea dhaifu, yenye magonjwa na mavuno kidogo. Kuchagua mbegu bora na kuzitibu na dawa za asili kabla ya kupanda huongeza ukuaji na mavuno ya choroko.
Ili kupata mbegu bora, anza kwa kuvuna mbegu kutoka kwa mimea yenye afya, na uzitandaze kwenye turubai. Chuja mbegu ili kuondoa mawe madogo na mbegu duni, kisha ubaki na mbegu bora pekee.
Matibabu ya mbegu
Unaweza kutibu mbegu kwa kutumia dawa za asili kudhibiti magonjwa yanayosababishwa na mbegu / udongo. Dawa hizo zinaweza kununuliwa kutoka kwa maduka ya wauzaji wa kilimo. Trichodema ni dawa ya kuvu inayotumiwa sana, hii husaidia ukuaji wa vijidudu vizuri karibu na mizizi. Mbegu pia zinaweza kupakwa na: mbolea ya kikaboni ili kuongeza ukuaji. Rhizobium, ambayo hutoa nitrojeni na kuiweka ardhini. Phosphate, ili kuongeza fosforasi kwenye udongo kabla ya kupanda.
Kabla ya kuanza kutibu mbegu, yeyusha nusu ya kiganja cha sukari nguru au sukari kwenye glasi ya maji. Weka kilo 1 ya choroko kwenye chombo. Nyunyiza trichodema kulingana na nusu ya kijiko cha chai, na kisha uchanganye mbegu. Ongeza vijiko viwili unusu vya rhizobia. Ongeza kipimo sawa cha fosfeti. Nyunyiza maji yenye sukari kwenye mbegu na uzichanganye. Kisha, kausha mbegu chini ya kivuli kwa saa 1 kabla ya kupanda.
Kutengeneza bidhaa ya asili
Changanya mikono 2 ya samadi ya ng‘ombe pamoja na nusu lita ya mkojo wa ng‘ombe, vijiko 3 vya chokaa, glasi 1 ya maziwa ya ng‘ombe au mtindi, na lita 10 za maji kwenye pipa ya plastiki.
Weka mchanganyiko usiku kucha, kisha koroga ukitumia kijiti cha mbao siku ifuatayo. Mchanganyiko huu unaweza kuhifadhiwa kwenye chombo kisichopenyeza hewa kwa mwezi 1.
Changanya kikombe kimoja cha mchanganyiko na kilo 1 ya mbegu. Vichanganye, na kisa vikaushie chini ya kivuli kabla ya kupanda.