Wakulima wengi hupoteza kiasi kikubwa cha mahindi kutokana na mbinu duni za kushughulikia nafaka baada ya kuvuna. Kufuata mbinu bora za kushughulikia mahindi baada ya kuvuna huongeza mavuno na pia hupunguza hasara.
Punje za mahindi zilizokaushwa vizuri huwa ngumu sana, na hutoa sauti ya mlio zinapomiminwa, na pia hazishikilie mkononi zinapobonyezwa. Hata hivyo, mahindi yanaweza kuvunwa yakiwa bado mabichi, iwapo hariri zimebadilika kuwa kahawia, na pia huvunwa kavu wakati majani na maganda yamekauka kabisa.
Hatua
Vuna mapema wakati safu nyeusi inapotokea kati ya punje na gunzi ili kupunguza uvamizi wa wadudu.
Ondoa maganda, na kisha pukuchua kwa mashine ili kuepuka kuvunja nafaka.
Kausha punje na zilinde dhidi ya mvua ili kuepuka shambulio la ukungu.
Daima hifadhi nafaka katika magunia na maghala ili kuepusha nafaka kuota mizizi.
Hifadhi mahindi katika sehemu safi iliyokavu, na weka kemikali za kinga.
Panga magunia ya mahindi kwenye mbao ili kuzuia ukuaji wa ukungu.
Nyunyiza kwa kutumia kemikali za Ak tellic ili kuepusha punje kushambuliwa na wadudu.