»Mbinu jumuishi za kudhibiti wadudu katika mitende (IPM)«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/date-palm-ipm

Muda: 

00:07:34
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Ministry of Agriculture, Iraq

Mitende hushambuliwa na wadudu wengi, lakini mikakati jumuishi ya kudhibiti wadudu kama vile; matumizi ya dawa za asili, upandaji mseto na utumiaji wa mitego ya mwangaza.

Awali, tunaweza kutumia dawa asili za kuua wadudu ambazo haziathiri mazingira. Hizi hutengenezwa kutoka kwa mitishamba. Unapotumia dawa za asili, hakikisha kwamba unasoma maagizo yaliyoandikwa kwa chupa, pamoja na kufuata miongozo ya kuchanganya na kunyunyiza dawa hizo. Pia, unafaa kuvaa vifaa vya kinga kama vile glavu. Bomba la kunyunyiza dawa lazima lisafishwa awali kwa maji safi kabla ya matumizi. Epuka kunyunyiza wakati wa hali ya upepo.

Kilimo mseto

Njia ya pili ni kupanda mseto, ambapo mboga kama vile figili hupandwa pamoja na mitende. Mboga huvutia maadui asili wa wadudu wa mitende, na kwa hivyo hudhibiti idadi kubwa ya wadudu.

Tatu, tunaweza kutumia mitego ya mwangaza, ambapo mitego hii hutumia mwangaza wa jua kukamata aina nyingi za wadudu. Kufanikiwa kwa njia hii kunategemea kuweka mitego mahali sahihi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:06mikakati jumuishi ya kudhibiti wadudu
01:0702:07Tumia dawa asili za kuua wadudu ambazo haziathiri mazingira (Oxymatrine).
02:0802:28Unapotumia dawa za asili, hakikisha kwamba unasoma maagizo na miongozo ya kuchanganya na kunyunyiza dawa hizo, na kuvaa vifaa vya kinga.
02:2902:48Bomba la kunyunyiza dawa lazima lisafishwa. Epuka kunyunyiza wakati wa hali ya upepo.
02:4904:05Kupanda mseto na mboga kwa mfano figili.
04:0606:25kutumia mitego ya mwangaza, ambapo mitego hii hutumia mwangaza wa jua kukamata aina nyingi za wadudu
06:2607:34Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *