Liche ya kuwa nafaka yenye lishe bora, ukuzaji wa mawele ni mdogo kutokana na mbinu duni zinazotumika ambazo husababisha ubora duni wa mavuno.
Mawele ni chanzo kikubwa cha virutubisho vinavyosaidia mwili wa binadamu kupigana na magonjwa. Uzalishaji wake unahusisha hatua kama vile; utayarishaji wa ardhi, kupalilia, kuweka mbolea, uvunaji, na utunzaji baada ya kuvuna.
Kilimo cha mawele.
Maandalizi ya ardhi yanapaswa kufanywa kwa kulima na kulainisha udongo mara mbili. Matuta na mitaro hutengenezwa iwapo utamwagilia, na ardhi hutayarishwa tambarare iwapo kilimo kitategemea mvua. Weka samadi ya mifugo. Samadi ya mifugo huongezwa kwa uwiano wa tani 8–10 kwa kila hekta.
Vile vile, panda kilo 3 za mbegu kwa kila hektar katika udongo mzuri, na kilo 4.5 kwa udongo duni huku ukiacha umbali wa sm 30 x 60 kutegemea umwagiliaji na rutuba ya udongo. Katika hali ya mvua, acha umbali wa sm 45 x 10–12 kati ya mbegu huku ukitumia njia ya kuchimba safu 6 ambayo husababisha idadi ya mimea kati ya laki 1.5–1.75 kwa kila hektar.
Tibu mbegu kwa azobacter au azospirillum ili kuongeza mavuno ya nafaka. Weka mbolea kama vile kilo 40–60 ya Nitrojeni kwa kila hektar, kilo 20–30 ya fosforasi kwa kila hektari, na potasiamu kwa mazao yanayotegemea mvua. Halafu kwa mazao yanayotegemea umwagiliaji, ongeza Nitrojeni 100–120 kg/ha, fosforasi 40–60 kg/ha na potasiamu. Weka nusu ya kiwango cha Nitrojeni wakati wa kupanda, na nusu nyingine huongezwa siku 45 baada ya kupanda. Ongeza fisforasi na potasiamu tu wakati wa hali ya mvua na umwagiliaji.
Umwagiliaji hufuatwa na kuandaa mitaro mipana, kulima kwa kina kirefu na kuweka samadi au mboji ili kusababisha matumizi bora ya maji. Palilia shamba kwa kuongoa magugu na kutumia na dawa ili kudhibiti magugu.
Tumia mfumo sahihi wa upandaji wa mimea kama vile mchanganyiko wa mazao, na kilimo mseto. Vuna mawele kwa kukata mmea mzima wakati kiwango cha unyevu wa punje ni 20% baada ya siku 85–95. Kausha nafaka kwa siku 2–3 ili kupunguza unyevu hadi 12% na kisha pura na kuhifadhi.
Magonjwa makubwa ni ukungu na ubwiri unga ambayo hudhibitiwa kwa kutibu mbegu, kulima kwa kina kirefu, kuepuka kupanda mmea mmoja, kunyunyizia dawa nakadhalika.
Aina za mawele ni pamoja na CZP-ic923, pusa comp 383, WCC75, HC10, HC20 na pusa comp 334.