Mshubiri ni chanzo kizuri cha virutubisho kama vile magnesiamu, shaba, zinki, sodiamu, kalsiamu, chuma, potasiamu na magnesiamu, na vitamini kama A, C, E, folic acid, B1, B2, B3, B6 na pia B12.
Mchakato wa kutengeneza mbolea
Pata majani ya mshubiri na utoe sehemu laini ilio katikati mwa jani.
Kata sehemu hiyo katika vipande vidogo, na pia kata sehemu ya kijani ya jani hilo katika vipande vidogo.
Ongeza lita 1 ya maji kwenye mchanganyiko na subiri kwa siku 7.
Baada ya siku 7, rangi ya maji itabadilika na sasa mchangnyiko huo ni mbolea tayari.
Chuja mchanganyiko , ongeza lita 5 za maji na nyunyizia mimea yako. Mbolea hiyo inaweza kutumika moja kwa moja kwenye majani ya mmea au kwenye mashina. Vile vile inaweza pia kunyunyiziwa kama dawa ya kuua wadudu.