Unaweza kutumia mawe kwenye shamba kwa kujenga mitaro.
Mara kadha, wakulima wana mawe mengi shambani mwao lakini kwa upande mwingine wana shida, kwamba mchanga unapungua mwaka hadi mwaka. Mvua huosha udongo kutoka ardhini ambayo husababisha udongo kuwa mwembamba, kavu na gumba. Hii ndio sababu mavuno yako yanaweza kuwa kidogo.
Ujenzi wa mitaro ya mawe
Unaweza kutumia mawe kutoka shamba lako kwa kujenga mtaro wa mawe. Mitaro husaidia kupunguza mtiririko kasi wa maji ya mvua hasa kwenye ardhi ilioteremka. Mitaro ya mawe husaidia kwa upenyezi wa maji kwenye mchanga na kwa hivyo, mimea hupata unyevu wa kutosha. Udongo hukusanyika kwenye mitaro. Kwa hivyo, shamba hupumzika vizuri. Mitaro ya mawe ina faida sana katika maeneo ambayo yana misimu mingi ya mvua na dhoruba nzito.
Hatua kwa hatua
Tafuta upande mmoja na utengeneze mitaro kidogo mahali popote unapotaka kuweka mawe. Ikiwa una shida kupata mahali pa kuweka mawe, uliza mtoa huduma ili kupata msaada.
Kisha unafanya mstari kando ya mtaro. Baadaye weka mtaro wa mawe. Hakikisha kuijenga kando ya mteremko bila kupanda au kushuka. Awali, jenga mawe makubwa kwa upande ulio chini zaidi na kisha ongeza mawe ya kati juuya mawe makubwa. Baadaye, ongeza mawe madogo juu, ili ushikilie vizuri. Kadri miaka inavyokwenda mawe yanaweza kuanguka chini, na unapaswa kuongeza mapya.
Baada ya miaka michache utagundua, udongo hukusanya kwenye mtaro. Hapo, magugu na mimea vina nafasi nzuri ya kukua. Katika kipindi cha miaka 20, unaweza kukusanya takribani udongo wa sentimita 30.
Kwenye mtaro pia unakusanya maji, ambayo huweka unyevu katika udongo. Kwa mfano unaweza kupanda mipapai hapo, kwa sababu wangepata maji ya kutosha.
Kujenga mitaro ya mawe ni kazi nzito, lakini hufanya kazi kwenye shamba kuwa rahisi. Itasaidia kuifanya ardhi yako iwe na unyevu na rutuba.