Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa bata hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Nyama ya bata ni ladha na ina wateja wengi sana. Katika miezi 3, bata dume huwa na uzito wa kilo 5. Ufugaji wa bata huhitaji nafasi ndogo na ni biashara yenye faida kubwa.
Usimamizi wa bata
Kwa usimamizi mzuri wa ufugaji wa bata, banda linapaswa kuwekwa katika maeneo iliyokaribu na maji ya kutosha. Kila bata huhitaji nafasi ya futi 4–5 za mraba. Vifaranga vya umri wa siku moja vinafaa kutunzwa ipaswavyo katika mahali maalum palipo na halijoto ya nyuzi joto 95 katika wiki ya kwanza. Punguza halijoto kwa nyuzi joto 5 kila wiki, na vifaranga hutunzwa katika eneo hilo kwa wiki 3–4 katika msimu wa kiangazi, na wiki 6–7 katika msimu wa baridi.
Vile vile, banda la vifaranga linapaswa kujengwe katika sehemu ambazo hazina unyevu. katika hili, tandaza pumba kavu za mpunga au pumba za mbao kwenye sakafu. Baada ya kuhesabu vifaranga, wape maji yaliyochanganywa na vitamini. Lisha kila kifaranga gramu 5 kila siku.
Kulisha bata kwa malisho bora ni muhimu, na malisho haya yanaweza kuwa ya asili, yaliyotengenezwa tayari au chakula cha kuku. Usiwape bata chakula kikavu, hivyo basi wape maji na chakula cha unga, na ulishe bata kwa muda wa wiki 6. Ili kufanikiwa na kuzaliana, hifadhi bata dume 1 kwa majike 5–9, na uwatolee chanzo cha maji.
Bata huathiriwa na kipindupindu. Wanaweza kuuzwa kwa miezi 3, na kiwango cha vifo ni kidogo sana. Bata huchanjwa ndani ya siku 25 na pia baada ya siku 40.
Bidhaa za bata zina wateja wengi sana. Anzisha mikakati uuzaji sokoni kabla ya kuanza kufuga bata.