»Mpango wa kibiashara wa ufugaji wa Kuku wa mayai «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=KXK_i6cPbxo

Muda: 

00:06:25
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English

Kwa kuwa ni biashara nzuri, ubora wa wingi wa bidhaa za kuku wa mayai hutegemea mbinu za usimamizi zinazotumika.

Kuku wa mayai wanahitaji kukuzwa kuanzia wakiwa na umri wa siku moja, na huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki 18–19, na huendelea hadi umri wa wiki 72–78. Kila kuku hutumia kilo 2.25 za chakula katika kipindi cha kutaga mayai.

Usimamizi wa kuku

Kwa kuwa ufugaji wa vifaranga katika wiki za kwanza baada ya kuzaliwa ni muhimu, tengeneza mfumo mzuri wa kuwatolea maji ya kunywa ya kutosha. Fundisha kuku kunywa maji yaliyochanganywa na asilimia 5 ya glucose kwa ajili ya kupata nishati.

Kata midomo ya vifaranga katika umri wa siku 8–10, na wiki 8–12 kwa kuku wanaokua. Kata midomo ya vifaranga kwa urefu wa 0.2cm kutoka puani, na sentimita 0.45 kutoka puani kwa kuku wanaokua. Kata midomo yote miwili kwa kutumia mashine yenye ncha kali. Usikate mdomo siku 2 baada ya kuchanja ndege, au baada ya kuwatibu au wakati hali ya hewa ni mbaya, na wakati kuku wanaanza kutaga.

Vile vile, tolea kuku maji safi ya kunywa kulingana na mahitaji. Safisha maji kwa kutumia dawa maalum, na tolea kuku maji baridi wakati wa msimu wa kiangazi na maji ya vuguvugu wakati wa msimu wa baridi. Ongeza kalsiamu, fosforasi, vitamini, na amino asidi vya kutosha kwenye chakula cha kuku kulingana na umri na ukubwa.

Wape kuku chakula chenye protini na madini mengi, na uwape kalsiamu asilimia 2% wiki 2 baada ya kuzaliwa, na kisha wape chakula cha kuanzia hadi wiki 4, na kisha walishe mara 2–3 kwa siku hadi wanapofikisha umri wa wiki 18. Lisha kuku kulingana na umri na uzito na usipunguze kiasi cha chakula wakati wa kutaga.

Katika umri wa wiki 20, asilimia 5% ya kuku huanza kutaga na asilimia 10% hutaga baada ya wiki 21 na hutaga sana katika wiki 26–30. Kiwango cha utagaji wa yai na saizi ya yai huongezeka polepole hadi kuku kufikia umri wa wiki 50.

Hatimaye panga mradi wa kuchanja ndege ili kuzuia magonjwa, na kuongeza ustahimilivu dhidi magonjwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:24Kuku wa mayai wanahitaji kukuzwa kuanzia wakiwa na umri wa siku moja.
00:2500:35Huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki 18–19
00:3600:57Kila kuku hutumia kilo 2.25 za chakula katika kipindi cha kutaga mayai.
00:5801:06Tengeneza mfumo mzuri wa kutolea vifaranga maji ya kunywa ya kutosha.
01:0701:25Fundisha kuku kunywa maji yaliyochanganywa na glucose
01:2601:38Kata midomo ya vifaranga katika umri wa siku 8–10, na wiki 8–12 kwa kuku wanaokua.
01:3901:52Kata midomo ya vifaranga kwa urefu wa 0.2cm kutoka puani, na sentimita 0.45 kutoka puani kwa kuku wanaokua.
01:5302:03Kata midomo yote miwili kwa kutumia mashine yenye ncha kali
02:0402:28Usikate mdomo siku 2 baada ya kuchanja ndege, au baada ya kuwatibu au wakati hali ya hewa ni mbaya , na wakati kuku wanaanza kutaga.
02:2902:39Tolea kuku maji safi ya kunywa kulingana na mahitaji.
02:4002:50Safisha maji kwa kutumia dawa maalum, na tolea kuku maji baridi wakati wa msimu wa kiangazi na maji ya vuguvugu wakati wa msimu wa baridi.
02:5103:03Ongeza kalsiamu, fosforasi, vitamini, na amino asidi kwenye chakula cha kuku kulingana na umri na ukubwa
03:0403:27Tumia dawa maalum kusafisha maji.
03:2803:38Wape kuku chakula chenye protini na madini mengi
03:3903:48Wape kalsiamu asilimia 2% wiki 2 baada ya kuzaliwa, na kisha wape chakula cha kuanzia hadi wiki 4
03:4903:57Walishe mara 2–3 kwa siku hadi wanapofikisha umri wa wiki 18
03:5804:18Lisha kuku kulingana na umri na uzito
04:1904:32Katika umri wa wiki 20, asilimia 5% ya kuku huanza kutaga na asilimia 10% hutaga baada ya wiki 21
04:3304:50Kuku hutaga sana katika wiki 26–30.
04:5105:16Kiwango cha utagaji wa yai na saizi ya yai huongezeka polepole hadi kuku kufikia umri wa wiki 50.
05:1706:14Hatimaye panga mradi wa kuchanja ndege
06:1506:25Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *