Kwa kupanda mbegu za mpunga moja kwa moja kwenye mistari, unaweza kutatua shida ya ukosaji wa maji wakati wa kupiga vidimbwi. Hii hufanyika katika vidimbwi na maeneo makavu pia.
Wakulima wengi hulima mara chache kabla ya kupiga vidimbwi, ambavyo huhitaji mvua nyingi. Kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, mvua huchelewa kunyesha na hivyo hakuna maji ya kutosha wakati wa kupiga vidimbwi. Hii husababisha mimea kuchelewa kukua, haswa katika shamba lenye mchanga mwepesi.
Kupanda mbegu za mpunga moja kwa moja
Chukua mbegu bora ili kupata mavuno mazuri. Unapotumia dawa za kuua magugu zisizochagua magugu kwa utaratibu, unaweza kudhibiti magugu ambayo yangeweza kuwa shida, haswa katika mwaka wa kwanza. Tumia madawa haya masaa matatu kabla ya kupanda, laa sivyo, utaua mbegu.
Panda mbegu kwenye mistari. Kwa hivyo, unaweza kutumia „lithao“ au zana ya kupanda inayounganishwa na zana ya kulima. Lithao ni kifaa ambacho hutumika kwa mikono. Zana hii hulima mitaro mitatu. Baada ya kutumia lithao, panda mbegu kwa mkono. Kwa kutumia kifaa hiki unahitaji udongo uliyolimwa vizuri, wepesi.
Zana ya kupanda mbegu inayounganishwa na zana ya kulima/mkombo hufanya kila kitu kwa hatua moja. Zana hii hufanya mitaro sita, hupanda mbegu na pia kuifunika kwa mchanga. Kifaa hiki ni nzuri kuokoa wakati na kupanda eneo kubwa.
Manufaa
Zao ambalo limepandwa kwa mbegu moja kwa moja huhitaji maji kidogo, kazi kidogo na pesa kidogo kuliko lile linalopandikizwa. Pia, mavuno yako yatakuwa tayari mapema kwa wiki 1-2.
Kwa kuvuna mapema, unaweza kupanda mazao yanayofuata mapema pia. Mazao ambayo unaweza kupanda wiki moja au mbili mapema ni: viazi, maharadali, ngano au mahindi ya msimu wa baridi. Unaweza hata kupanda zao la tatu.