Ili kufanikiwa na ufugaji wa kuku wa nyama, unapaswa kuwapa chakula sahihi ipaswavyo.
Kuku wa nyama hula chakula kingi lakini si kanuni ya jumla kwamba kadiri chakula kinavyoliwa ndivyo matokeo yanavyokuwa bora. Ili kutumia kwa ufanisi chakula kinacholiwa na ndege, unapaswa kuongeza uwiano wa ubadilishaji wa malisho (FCR) ambao hulinganisha kiasi cha chakula kinacholiwa na uzito unaowekwa na ndege. Uwiano wa ubadilishaji wa malisho ni wa juu zaidi kwa ndege wachanga lakini hupungua kadri ndege wanavyokua.
Kuongeza uwiano wa ubadilishaji wa malisho
Ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya malisho ya kuku wa nyama, unahitaji kuanzisha ratiba ya kulisha ambayo inahusisha kuwapa ndege malisho kila wakati, na wakati mwingine kusitisha kuwapa chakula kwa muda fulani.
Wakati wa wiki ya 1,2 na 3, lisha ndege sana kwa sababu katika wakati huu uwiano wa ubadilishaji wa malisho huwa juu kumaanisha kwamba chakula kidogo kinacholiwa husababisha ongezeko kubwa la uzito wa mwili.
Baada ya wiki ya 3, unaweza kusitisha kuwapa chakula wakati wa joto la mchana (11am hadi 4pm), na baadaye uwalishe jioni na usiku hadi asubuhi ufuatao. Kusitisha kulisha kuku kusizidi masaa 6 kwa sababu, laa sivyo kunaweza kupunguza uzito wa ndege.
Usimamizi wa kuku
Daima tolea kuku maji safi kila wakati. Kufanya huku ni rahisi unapotumia vihori vya maji viliyoboreshwa.
Hakikisha unawapa kuku maji baridi hasa wakati wa joto ili kupoza miili yao. Hii huzuia mafadhaiko na kifo cha ghafla.