Parachichi ni tunda lenye lishe kwa walaji na ni chanzo cha mapato. Hata hivyo, sehemu kubwa ya parachichi huharibika baada ya mavuno kwa sababu wakulima wengi wana ujuzi duni au hawana ujuzi wowote kuhusu jinsi bora ya kuvuna.
Kujifunza jinsi ya kuvuna parachichi hupunguza hasara baada ya mavuno na kusababisha ongezeko la mapato kwa wakulima. Zana zinazohitajika wakati wa mchakato wa kuvuna ni mikasi, magunia, na glavu ambavyo huzuia matunda kupata michubuko.
Mchakato wa kuvuna
Shikilia na ukate tunda ukiacha kijiti kilicho na urefu wa 1mm ili kurefusha maisha ya tunda wakati wa kuhifadhi.
Weka matunda kwenye gunia la kuvunia na mara baada ya gunia kujaa, weka matunda kwenye kreti. Weka kreti juu ya ardhi ili kudumisha usafi.
Pima uzani wa matunda yaliyovunwa ili kufuatilia kwa urahisi kiasi kilichovunwa shambani.
Panga makreti bila kuzidi kreti 5 juu, na uweke kreti tupu chini. Makreti yanayotumika kuvunia yasitumike kwa uuzaji wa bidhaa.
Usijaze kreti kupita kiasi. Hifadhi matunda yaliyovunwa kwenye kivuli ili kuepuka matunda kuchubuliwa.
Safirisha matunda mara tu kwenye eneo la kuhifadhia ili kudhibiti uharibifu.