Hali ya afya ya kuku huathiri uwezo wao wa kuzalisha mayai na nyama, jambo ambalo huathiri mapato na lishe ya wafugaji.
Nyama na mayai ya kuku yana asilimia kubwa ya protini na huzalisha kipato kikubwa kwa wafugaji. Maji machafu ya kunywa, mazingira machafu na malisho duni husababisha magonjwa ya kuku.
Usimamizi wa asili
Kuku wanapougua, huacha kuzalisha mayai na wengine hufa. Hata hivyo, kusafisha eneo kila siku na kuondoa chakula kilichobaki na chakula kilichoharibika, na kuhakikisha kuku wanapata maji safi ya kunywa kila wakati kunaweza kupunguza matukio ya magonjwa. Vile vile, ongeza poda ya maziwa na dawa ya permanganate ya potasiamu katika maji, na pia wape kuku chakula kilichosawazishwa ambacho kimechanganywa na vitunguu saumu. Unaweza pia kuwapa vitunguu saumu mara moja au mbili kwa wiki.
Vile vile, wape ndege majani na dawa ya kuua minyoo mara moja kwa mwezi. Dawa ya kuua minyo inaweza kuwa utomvu wa papai uliochanganywa na maji. Ili kupata mayai bora, ongeza kalsiamu kwenye malisho na uzuie vimelea vinavyoweza kusababisha kuwasha kwa ndege, kudondosha manyoya, upungufu wa damu na vifo.
Mwishowe, ondoa nyasi na uweke nyasi mpya kwenye banda, na zinyunyizie dawa.