Ubora wa matunda ya mbuyu unaweza kuathiriwa sana iwapo matunda hayatashughulikiwa vyema wakati na baada ya kuvuna. Usimamizi mzuri hupanua mapato ya wakulima.
Mabuyu hutumiwa kutengeneza vitafunio. Juisi ya mabuyu ni yenye afya, na inaweza kuongezwa kwa uji na michuzi. Ili kuvuna usipande mti, bali tumia kijiti kirefu kilicho na ndowano . Acha matunda kwenye mti kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kuhakikisha kwamba maganda yamekomaa vyema na ni makavu. Hii husaidia kuzuia ukungu kukua ndani ya tunda.
Kushughulikia mabuyu
Epuka matunda ya zamani ambayo yana rangi nyeusi, kwa hivyo vuna tu mabuyu kutoka msimu wa sasa. Kusanya tu matunda yaliyokomaa ambayo hayana uharibifu wote wala hayaja athiriwa na wadudu. Weka mabuyu kwenye mifuko safi kwa usafirishaji. Weka matunda kwenye mirundo midogo katika eneo safi lenye hewa nzuri ili hewa iweze kuzunguka kwa urahisi kuzuia ukuaji wa ukungu. Kagua na kugeuza matunda kwenye rundo mara kwa mara ili kuepusha unyevu.
Osha mikono kabla ya kushughulikia matunda. Wakati wa kuuza, pasua matunda, na kuondoa massa makavu pamoja na kuondoa nyuzi zilizoshika mbegu. Mara moja, weka massa kwenye gunia safi kuepusha uchafuzi.