Maembe yana ladha tamu na ni chanzo cha mapato kwa wakulima. Hata hivyo, kiasi kikubwa cha maembe huharibika kwa sababu ya utunzaji duni wakati na baada ya kuvuna. Maembe yakishughulikiwa vizuri, uharibifu utapungua.
Vuna maembe yaliyokomaa kwani matunda machanga yana ladha kali, na yale yaliyoiva sana yanaweza huharibika haraka. Hata hivyo, kabla ya kuvuna kata tunda ili uangalie rangi ya nyama ya tunda. Uvunaji unapaswa kufanywa kutoka 3:00 asubuhi hadi saa 9 mchana ili kupunguza mtiririko wa utomvu.
Hatua za usimamizi
Tumia kifaa cha kuvunia kilicho na ncha kali, na watu 2 ili maembe yasidondoke chini wakati wa kuvuna.
Ili kuvuna, kata tunda kwa namna inayobakisha kijiti cha 1 – 2 cm ili kusaidia kutiririsha utomvu. Weka maembe yaliyovunwa huku upande wa kijiti ukielekea chini kwenye sehemu safi ili kuepuka viini. Acha maembe yakae kwa saa 1 kisha ukate mabua au vijiti.
Tenganisha maembe yaliyochubuka kudhibiti uharibifu kwa mazuri. Weka kwenye vyombo vigumu ili kuzuia maembe yasibonyee na kuharibika.
Uza maembe kabla ya siku 2 kuisha kwa hivyo, tafuta soko kabla ya kuvuna.
Hifadhi maembe katika chumba kikavu kisicho na joto. Safirisha maembe kwenye kreti ili yasichubuke.