Tunahitaji mizinga, kisu, msumeno wa kupogolea, na sharubati ya sukari ambayo ina viwango vya sukari 50% na maji 50%. Nyunyiza sharubati hiyo kwenye nyuki.
Maji ya sukari huwapoza, huwapa virutubisho na vile vile kuwafanya kuwa mzito. Hii huwafanya kuanguka kwa urahisi tunapotikisa tawi la mti. Nyunyiza fremu za mzinga na sukari, hii husaidia kuchochea nyuki kuingia kwenye mzinga bila kuondoa fremu. Watikise nyuki kutoka kwenye tawi hadi kwenye sanduku la mzinga. Unapotikisa hakikisha malkia hadondoki, ikiwa malkia yuko kwenye sanduku nyuki vibarua watamfuata. Pindua kifuniko cha ndani juu chini ili kutolea nyuki waliobaki juu ya mzinga nafasi ya kutosha. Weka maji ya sukari kwenye ubao wa kuingililia mzinga, na funika kisanduku kwa kifuniko cha nje mara tu unapothibitisha kuwa malkia yuko ndani ya kisanduku.