»SLM01 Mistari/Mitaro ya mawe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/slm01-stone-lines

Muda: 

00:07:35
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Countrywise Communication, CIS Vrije Universiteit Amsterdam.

Ukame umesababisha uharibifu wa ardhi na changamoto nyingi katika maeneo kadha. Hata mvua ikinyesha, maji hutiririka kwenye udongo ulioganda huku yakibeba virutubisho.

Kwa bahati nzuri, mawe yanaweza kupangwa kwenye ardhi iliyoteremka ili kupunguza mtiririko kasi wa maji, pamoja na kutumika kama mfumo wa kuvuna maji. Mitaro ya mawe husaidia kuboresha rutuba ya ardhi tena, na pia kusababisha ukuaji wa mimea.

Ujenzi wa mitaro ya mawe

Anzisha mstari kwa eneo sawiya ukifuata mwinuko wa ardhi. Kisha chimba msingi wa mtaro ambapo mawe makubwa huwekwa kwanza, yakifuatiwa na madogo.

Jenga mtaro wa mawe uliyo na urefu wa 25 cm hadi 30 cm. Mitaro ya mawe husaidia kwa upenyezi wa maji kwenye udongo. Na pai hupunguza mtiririko kasi wa maji ya mvua pamoja na kukusanya udongo. Hii hupunguza mmomonyoko wa udongo na hukusanya maji yanayohitajika kwa mmea ili kunawiiri.

Iwapo mawe ni machache, panda nyasi ambayo husaidia kuboresha ufanisi wa mtaro wa mawe.

Faida

Mitaro ya mawe ni rahisi kujenga na gharama yake ni nafuu. Pia inahitaji matengenezo kidogo. Mitaro ya mawe ni msingi ambao mbinu mbalimbali za uhifadhi na uzalishaji hujengwa.

Mabadiliko ni ya kushangaza baada ya muda kwani mistari ya mawe hufanya kama mfumo wa kuvuna maji na hurejesha rutuba ya ardhi duni, na hivyo kuanzisha tena mimea.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:40Ukame umesababisha uharibifu wa ardhi
00:4101:00Tumia mawe kutengeneza mtaro ambao husaidia kupunguza mtiririko kasi wa maji.
01:0101:40Jenga mtaro wa mawe uliyo na urefu wa 25 cm hadi 30 cm.
01:4102:20Anzisha mstari kwa eneo sawiya ukifuata mwinuko wa ardhi. Kisha chimba msingi wa mtaro ambapo mawe makubwa huwekwa kwanza, yakifuatiwa na madogo.
02:2103:15Panda nyasi ambayo husaidia kuboresha ufanisi wa mtaro wa mawe.
03:1604:10Tumia mawe katika kujenga mtaro wa mawe.
04:1005:08Mitaro ya mawe hufanya kama mfumo wa kuvuna maji na hurejesha rutuba ya ardhi duni, na hivyo kuanzisha tena mimea.
05:0906:37Kudumisha mitaro ya mawe
06:3807:35Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *