Uharibifu wa ardhi huleta tufani za vumbi zinazosababisha jangwa. Upandaji wa miti unaweza kutumika kama njia ya kupunguza athari za jangwa.
Kuanzisha miradi ya upandaji wa miti aina za kigeni kama vile mikaratusi na mipaina haifanyi vizuri katika maeneo ya ukame. Miti ambayo inaweza kustahimili na kuishi katika maeneo kame ni miti ya asili ambayo hutunzwa na wakulima.
Uhuishaji
Uhuishaji asili wa ardhi kupitia wakulima hufanywa kwa kuchagua miti iliyo na mashina ambayo yamenawiri zaidi na hivyo kusaidia miti hiyo kukua vyema ili kuhukumu aina bora ya uhuishaji. Hii inahitaji uzoefu pamoja na maarifa.
Miti yenye nguvu zaidi ambayo imebaki kwa miaka kadha huchaguliwa na kukatwa kwa mashina. Baadaye, miti michanga huchipuka kutoka kwenye mashina ikipata maji.
Umuhimu wa miti
Miti huzuia mmomonyoko wa ardhi unaosababishwa na upepo na maji. Miti huboresha muundo wa udongo kwa hivyo kurejesha rutuba ya udongo. Hii huruhusu kutekeleza kilimo endelevu.
Miti ya asili pia inaweza kutumika kama kuni wakati wa ukame, lakini itakua tena wakati mvua itakapoanza kunyesha.
Miti husaidia kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.