Kilimo cha uhifadhi ni muhimu kwa kupanua na kuboresha mazao.
Kwa sababu ya kuendelea kulima bila kuboresha ardhi, udongo umepoteza rutuba na vile mavuno yamekuwa machache. Unaweza kutumia mbinu ya kilimo cha uhifadhi ili kulinda udongo dhidi ya mmomonyoko. Kilimo hiki kinategemea kwa nguzo tatu: 1. Usumbufu uchache wa udongo ili kudhibiti mmomonyoko wa ardhi. 2. Unapanda jamii ya kunde kwa mzunguko, amabayo husaidi udongo kupata nitrojeni. 3.Unafaa kufunika udongo, kwa kuacha mabaki ya mimea shambani baada ya kuvuna.
Kulima kilimo cha uhifadhi.
Kwa kwanzia, mashimo madogo huchimbwa baada ya kuvuna. Mashimo hayo hutengenezwa kila mwaka. Mashimo hayo yanafaa kuwa wa upana wa sentimita 15, urefu wa sentimita 30 na kina cha sentimita 15. Acha umbali wa sentimita 79 kati ya mashimo, na sentimita 90 kati ya kila safu.
Unaweza pia kupiga mitaro ukitumia mafahali. Maanake, udongo ulio kwenye mtaro au shimo pekee ndio inaosumbuliwa kwa kulima. Nafasi zilizokati zinaachwa. Hii hudumisha mpangilio wa mchanga na utanzaji wa viumbe hai ardhini. Baada ya kutayarisha shamba, weka mbolea na chokaa kimaususi katika mashimo hayo au mitaro kisha rejesha udongo. Shamba hutayarishwa wakati wa kiangazi . Hii huruhusu upanzi kwa mda unaofaa mara tu mvua inaponyesha.
Kubadilisha mazao kila mwaka.
Kubadilisha mazao ni hatua muhimu. Kila msimu, mimea inaopandwa hubadilishwa ili kupunguza wadudu na magonjwa, na kudumisa rutuba kwenye udongo. Kwa mfano, badilisha mahindi ikifuatiwe na jamii kunde kama vile maharagwe , soya au karanga. Katika msimu ufuatao, panda mimea wa kuuzwa kama vile pamba.
Funika shamba kwa matandiko ya mabaki ya mimea kwa mwaka mzima .Hii huzuwia mmomonyoko wa ardhi wataki wa mvua. Kadri muda unavyopita, matandiko hayo huoza na kuongeza rutuba.
Njia nyingine ni kupanda miti shambani. Miti ya mgunga au mkababu huchukua nitrojeni kutoka hewani na kuiweka ardhini kupitia kwenye mizizi. Mgunga au Mkababu pia huitwa mti mbolea. Katika msimu wa upanzi, matawi yake huongeza virutubisho udongoni yanapoanguka. Kwa sababu ya kudondosha majani, hatua inaruhusu mwangaza wa jua hufikia mimea. Mizizi ya mti huo hufikia maji ardhini na kwahivyo haushindani kupata unyevu au virutubisho vilivyo katika udongo wa juu.