Wingi na ubora wa mtama huamuliwa na ubora wa mbegu na mbinu ya uzalishaji.
Mtama ni zao la tano muhimu katika nchi zinazoendelea, na hukuzwa katika maeneo kame, yalio na mvua kidogo, na ukame. Mtama hukuzwa katika msimu wa mvua na baada ya mvua. Ni chanzo cha chakula kwa wanyama katika mfumo wa kilimo cha mchanganyiko wa mazao na mifugo.
Uzalishaji wa mtama
Mtama hustawi katika unyevu uliosalia kwenye udongo, na una tija wa mara 7 kwa hekta. Hii hufanywa kwa kuchagua udongo unaofaa baada ya kuvuna kunde. Tayarisha ardhi kwa kutengeneza mitaro ili kuhifadhi unyevu wa kutosha wakati wa msimu wa upandaji.
Pili, tibu mbegu kwa kutumia kemikali ili kuzilinda dhidi ya shambulio la wadudu na magonjwa. Panda kilo 10 ya mbegu kwa kila hektar. Tengeneza mitaro na weka mbolea huku ukiacha umbali wa sentimita 45×15 kati mimea.
Weka mbolea; kilo 40 ya nitrojeni, na kilo 20 ya fosforasi wakati wa kupanda, na nyunyiza dawa ya kuua magugu baada ya kupanda. Dhibiti magugu na wadudu kwa kunyunyizia dawa siku 25–30 baada ya kupanda. Mtama hukomaa kati ya siku 110–120, hata hivyo huvunwa siku 15 kabla ya siku za kawaida za kuvunia.
Faida za mtama
Mtama hutumika kama chakula kikuu, huku unga wake hutumika kutengeneza chapati, uji, mikate, na malisho ya mifugo. Pia hutumika katika mfumo wa kilimo cha mazao na mifugo ambapo mitama yote huvunwa na mabua huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye.
Hatimaye, hutumika pia kama chakula, malisho, fumuele, na mazao la madhumuni mbalimbali.