Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa kware hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Nyama ya kware na mayai ni ya ubora wa juu kuliko mayai ya ndege wengine kwani yana protini nyingi, fosforasi, chuma, vitamini A, B1 na B2. Kware wanaweza kufugwa kwenye maeneo mbalimbali kama vile paa za nyumba.
Usimamizi wa kware
Ufugaji wa kware hutoa kipato na chakula. Ni chanzo cha ajira ambacho kinahitaji gharama ya chini, nafasi kidogo, chakula kidogo na wakati kidogo. Kuna wateja wengi wa bidhaa za kware.
Vile vile, kuna mbinu mbalimbali za ufugaji wa kware ambazo ni pamoja na mfumo wa kuhifadhia ndege ndani ya banda kwenye sakafu iliyotandikwa, na mfumo wa kutumia vizimba. Katika mfumo wa kwanza, taka, mchanga, majivu na pumba za mbao huwekwa kwenye sakafu.
Baada ya wiki 2, weka kware katika vizimba ili wapate uzito mzuri wa mwili. Watolee nafasi ya kutosha katika vizimba, na panga vizimba hadi 6 juu. Kunaweza kuwa na vizimba 4–5 kwa safu. Hatahivyo, hahikisha kwamba kizimba cha chini kina miachano kati ya mbao kwa usafishaji rahisi wa kinyesi. Weka vihori vya chakula mbele ya vizimba. Wape vyakula vilivyosawazishwa ili kuimarisha afya yao na tija. Chakula cha vifaranga kinapaswa kuwa na asilimia 27% ya protini, na chakula cha ndege wazima kiwe na asilimia 22%-24% ya protini. Kwa kware wa umri wa miezi 6, walishe gramu 30–35 za chakula kila siku.
Masaa 14–16 ya mwanga wa jua yanahitajika kila siku ili kuongeza uzalishaji wa yai na uzazi. Kwa kware dume, watolee mwanga kwa masaa 8 kila siku. Weke kware dume na majike pamoja ili kutaga mayai. Kusanya mayai kwa ajili ya kuanguliwa siku 4 baada ya kuwaweka majike pamoja na dume. Wape maji safi na chakula chenye lishe. Toa halijoto ya nyuzijoto 95 katika banda la vifaranga katika wiki ya kwanza, na nyuzi joto 90 katika wiki ya pili. Halijoto hii hupunguzwa hadi nyuzi joto 75 katika wiki ya tatu, na hatimaye nyuzi joto 60 katika wiki ya nne.
Leta vifaranga walioanguliwa kwenye chumba cha kuwatunzia ndani ya saa 24, na uwape maji yaliyochanganywa na glukosi. Tunza kware ipasavyo kwa kuzuia magonjwa, kwani vifaranga hawastahimili mabadiliko ya hali ya hewa na joto.