Ufugaji wa nguruwe ni biashara yenye faida kutokana na mahitaji makubwa ya nguruwe na bidhaa zao za protini. Hata hivyo, wakulima wanapaswa kudumisha kiwango cha juu cha usafi ili kudhibiti na kuzuia magonjwa.
Kuhakikisha kanuni bora za usimamizi ni muhimu sana kukomesha uingizaji wa magonjwa shambani. Kanuni hizi ni pamoja na; kuzungusha shamba na uzio, kuweka eneo la kuoshea miguu, kuosha mikono na kubadilisha nguo kabla ya kutembelea shamba, pamoja na kuzuia kutembelea shamba mara kwa mara. Jenga banda sahihi na uwe na maarifa ya kimsingi juu ya usimamizi wa nguruwe ili kufanya maamuzi mema kwa wakati. Daima kuwa na fedha ya kutosha kujenga banda, kununua malisho na madawa, kwa vile malisho bora husababisha wananguruwe wenye afya .
Faida za ufugaji wa nguruwe
Wafugaji hufuga nguruwe kutokana na faida mbalimbali zinazohusishwa mbazo ni pamoja na uwezo wao kuzaa watoto wengi. Pia ni mradi nafuu kusimamia kwani nguruwe wanaweza kula vyakula mbalimbali ambavyo pia hununuliwa fedha kidogo, kwani unaweza kupanda mazao yako ambayo yanaweza kutumika katika utayarishaji wa malisho.
Nguruwe hutumia vyema malisho katika ujenzi wa mwili na hivyo husababisha matokeo ya haraka. Vile vile, nguruwe ni sugu dhidi ya magonjwa iwapo usafi unadumishwa sana. Bila shaka, nyama ya nguruwe huhitajika sana kutokana na protini yake, na hivyo ina soko la tayari.