Barani Afrika, muhogo ni moja wapo ya mazao makuu yanayolimwa kwa kiasi kikubwa kwa chakula na mapato, kwa wakulima na wazalishaji.
Ugonjwa wa batobato ni moja wapo ya magonjwa muhimu ambayo huathiri uzalishaji.
Dalili za ugonjwa
Ugonjwa huo husababishwa na virusi vya muhogo vinayosambazwa na nzi weupe.
Mimea yaliyoathiriwa na ugonjwa huo inaweza kutambuliwa kwa madoadoa/ mabaka mepesi ya kijani au manjano kwenye majani. Pia, kwa majani madogo na yaliyoharibika.
Ugonjwa huo hauna tiba lakini unaweza kudhibitiwa.
Udhibiti wa ugonjwa
Tumia vipanda vya mihogo kutoka kwa wazalishaji waliothibitishwa. Panda aina za mihogo zinazostahimili magonjwa. Fanya kilimo cha mzunguko wa mazao ili kukomesha mzunguko wa magonjwa. Ng‘oa na kuchoma mimea yote yaliyoathiriwa na ugonjwa.
Panda aina moja shambani kwa wakati mmoja.
Daima, kagua shamba lako kwa ushambuliaji wa magonjwa.
Epuka kutumia vipanda vilivyoathiriwa wakati wa kuanzisha shamba.
Chukua vipanda kutoka kwa wazalishaji na wakulima waliothibitishwa.
Pata ushauri kutoka kwa watoa huduma wa ushauri. Mafunzo hutolewa na mashirika ya utafiti.