Kideri ni ugonjwa wa ndege unaosababishwa na virusi, ambao hauna tiba. Ugonjwa huu huenea kwa haraka sana kutoka kwa ndege walioambukizwa hadi ndege wenye afya ambao hawajachanjwa, na unaweza kusababisha vifo hadi asilimia 100.
Mojawapo ya dalili za ugonjwa wa kideri ni kujipinda shingo na kuyumbayumba katika mwendo. Ugonjwa wa kideri huathiri mfumo mkuu wa mishipa, na hivyo kusababisha ndege kuyumbayumba katika mwendo.
Kupungua kwa uzalishaji wa mayai
Ugonjwa wa kideri huathiri uzalishaji wa mayai. Hupunguza uzalishaji wa mayai, na husababisha na uzalishaji wa mayai yenye kasoro, mayai yenye maganda laini, na mayai yenye maji maji. Pengine, ndege hutaga mayai yasiyo na gamba, na katika hali mbaya ndege hutaga kiwiliwili. Yai la kawaida huwa na kiini chake katikati ya maji, wakati kuku aliye na ugonjwa wa kideri hutaga yai lililo na kiini kilichotenganishwa na maji ya yai.
Dalili zingine
Kutetemeka, udhaifu na kukunja mabawa ni dalili za kawaida katika kuku wa mayai. Viungo vya miguu hupooza. Kwa ndege ambao wamechanjwa awali lakini wameshambuliwa na aina tofauti ya ugonjwa wa kideri, mguu mmoja tu hupooza. Pia miguu yote hupooza kabisa na huonekana kama kijiti kilichokauka.
Ndege hushindwa kutembea ambapo miguu na mabawa yote yamepooza. Ndege pia hushindwa kusimama, kutembea, wala kutumia mabawa.
Mafadhaiko, ambapo ndege huonekana kuwa katika hali ya kukaa na kusinzia kila wakati, huku jicho moja au yote mawili yakifungwa kila wakati.
Kuhema, kukohoa na kuhara. Ndege walioathiriwa na ugonjwa wa kideri kutoa kinyesi cha maji ya kijani kibichi na damu.